Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Said Sidde amewataka wana CCM wa kata ya Ilala kujenga umoja na mshikamano wakati Chama Chama cha Mapinduzi kikielekea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 na a uchaguzi mkuu 2025.
Mwenyekiti Sidde alisema hayo Mtaa wa Kalume wakati Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Hajji Bechina alipokuwa akigawa kadi za Bima ya afya 300 na meza za Walimu wa shule ya Msingi Ilala Boma na Mkoani wilayani Ilala.
“Chama chetu kinaelekea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani hivyo akuna budi kujenga umoja na Mshikamano Ilala muache kugombana badala yake mfanye kazi za kujenga chama na kudumisha umoja na mshikamano “alisema Sidde .
Aliwaomba viongozi wa chama kata ya Ilala kujenga mshikamano muwe wamoja wasaidie Serikali chama kionekane siasa za chama cha Mapinduzi kwani Ilala miongoni mwa kata nane hivyo shughuli za chama zifanyike.
Alisema anaona Fahari kubwa maendeleo ya Ilala yanafanyika vizuri katika utekelezaji wa Ilani ukiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu na Diwani wa Kata Saady Khimji ambapo kwa sasa Ilala inakuwa ya kisaaa zinajengwa barabara mpya ni juhudi za Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Alisema Bungoni wanajenga Zahanati, Ilala Boma wanajenga mradi mkubwa soko la kisasa hivyo aliwataka wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali.
Wakati huo huo alitumia fursa hiyo kumpongeza Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kalume Hajji Bechina kwa kazi nzuri anayofanya katika kuisaidia Serikali na chama utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.
Alisema Mwenyekiti Hajji Bechina ni Mwenyekiti Bora ni miongoni mwa Wenyeviti 159 anafanya kazi kubwa za kijamii na kujituma katika Shughuli mbali mbali ikiwemo kuleta maendeleo katika mtaa wake.
“CCM Wilaya Ilala itampa ushirikiano Hajji Bechina katika shughuli zake zote za maendeleo pia nampongeza Diwani wa Kata ya Ilala Saady Kimji kwa kazi kubwa anayofanya za maendeleo na kutatua kero mbali za wananchi “alisema
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi