January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti Neema awataka UWT kujitokeza Kongamano Machi 19

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT Wilaya ya Ilala Neema Kiusa , amewataka Wanawake wa UWT kujitokeza kwa wingi katika kongamano la UWT Taifa viwanja vya Mnazi Mmoja Wilayani Ilala kumpongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt,Samia Suluhu Hassan .

Mwenyekiti Neema alisema hayo katika ziara zake na Kamati ya Utekekezaji UWT Wilaya Kata ya Kipunguni Wilayani Ilala na Kata ya Kivule ziara ya kuwashuru Wanachama pamoja na kuangalia uhai wa Jumuiya hiyo ambapo kila Kata inajizolea Wanachama wapya .

Mwenyekiti Neema Kiusa alisema katika kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Umoja wanawake UWT Taifa Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan .

“Nawaomba wanawake wenzangu wa Wilaya ya Ilala kujitokeza kwa wingi Katika kongamano letu siku ya Machi 19 Jumapili Viwanja vya Mnazi Mmoja tuje kuongea na Mwanamke mwezetu na kumpongeza mama jambo la mama ni letu sote “alisema Neema .

Mwenyekiti Neema aliwataka Wanawake wa UWT kupeana Taarifa kuhusiana na kongamano hilo la UWT ambalo linafanyika Ilala .

Akizungumzia mwendelezo wa ziara ya Kamati ya utekekezaji ya Wilaya alisema dhumuni la ziara hiyo uhai wa JUMUIYA ya Umoja wanawake pamoja na kuwashukuru wanachama wao .

Mwenyekiti Neema aliwataka Wanawake kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi wa serikali za Mitaa mwaka 2024 majina yao yatapewa kipaumbele kwa wale wanaoshiriki kazi za chama na kujitoa .

Aliwataka Wanawake wa Uwt Wilaya ya Ilala kufuata kanuni na taratibu za chama katika utekelezaji wa majukumu yao .

Wakati huo huo aliwataka Wanawake wa UWT kujitolea na kujenga mahusiano ndani na nje ya chama hila wasifanye siasa chafu za kupanga safu za Madiwani na Wabunge Kwani wakati wake bado wa kupanga safu hizo kwa Sasa watumikie chama katika utekelezaji wa Ilani na kumsaidia RAIS kutangaza miradi mbalimbali ya Maendeleo .

Mwenyekiti wa umoja wanawake Wilaya ya Ilala NEEMA Kiusa (katikati )akiwa na Viongozi wa Kamati ya utekekezaji Wilaya ya Ilala katika ziara ya kuwashukuru Wanachama kata ya Kipunguni na Kivule.
Mwenyekiti wa umoja wanawake UWT WIlaya ya Ilala Neema Kiusa akiwakabidhi kadi wanachama wa UWT Kata ya Kipunguni katika ziara ya kuwashukuru wanachama
Wanachama wapya wa umoja wanawake UWT wakila kiapo baada kuapishwa Kata ya Kipunguni wilayani Ilala katika ziara ya kamati ya utekekezaji
Kaimu Katibu wa umoja Wanawake Wilaya ya Ilala Mariam Bakari akizungumza na Wanawake wa Kipunguni wakati wa ziara ya kamati ya utekekezaji Wilaya ya Ilala kuwashukuru wanachama na kuangalia uhai wa Jumuiya(aliyekaa )Mwenyekiti wa Uwt Wilaya ya Ilala Neema Kiusa.
Mwenyekiti wa Umoja wanawake Uwt Wilaya ya Ilala NEEMA Kiusa akizungumza na Wanawake wa Uwt Kipunguni katika ziara ya kuwashukuru wanachama