January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti Mushi aipongeza Idara ya maendeleo ya jamii Ilala

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Morogoro

MWENYEKITI wa Kamati za Huduma ya Jamii Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Steven Mushi, ameipongeza Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kuviwezesha vikundi kupewa mikopo ya Serikali.

Mwenyekiti Mushi aliyasema hayo katika maonyesho ya Wakulima nane nane Kanda Mashariki Morogoro ambapo Halmashauri ya Jiji imeibuka kidedea kushika nafasi ya kwanza kundi la halmashauri za Miji na manispaa.

“Idara yangu ya Maendeleo ya Jamii naipongeza kwa kufanya vizuri katika mikopo ya asilimia kumi ya Wanawake Vijana na Watu Wenye Ulemavu vikundi vingi vimepewa mikopo vikiwemo vilivyo Shiriki maonyesho ya Wakulima nanenane katika Banda la Ilala ” alisema Mushi.

Aidha Mushi alitumia fursa hiyo kuipongeza Idara ya Kilimo na Uvuvi ya Halmashauri hiyo kwa ushindi mkubwa wa vikombe walivyopata katika Maonyesho hayo .

Alisema Jiji letu la Dar es Salaam limeibuka KIDEDEA katika usafi katika majiji Bora ,vilevile katika mashindano ya Umoja wa Shule za Msingi UMITASHUMTA ILALA imeshika namba Moja na Leo tuzo hizi za Idara ya Kilimo ni mafanikio Bora kwa Wana Ilala nyota inaendelea kungara Wilaya yetu ya Ilala.

Aliwataka wakuu wa Idara na Watumishi kushirikiana na kujenga umoja sambamba na kushirikiana katika kuleta maendeleo .

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji Arndo Mwakuga alisema ushindi wa Wilaya ya Ilala Kwa ajili ya ushirikiano wa Wakuu wa Idara,Madiwani na Watumishi pamoja na Idara ya Kilimo .

Kaimu Arndo aliwataka wawe wamoja na kujenga Wilaya ya Ilala kwa ajili ya Maendeleo na kupeana na ushauri.

Diwani wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Saada Mandangwa aliwapongeza Watumishi ,Wakuu wa Idara na Madiwani Kwa Ushirikiano wao Katika kufanikisha ushindi Katika sekta ya Kilimo na Uvuvi.