December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti Jumuiya ya Maridhiano awaasa wananchi kusikiliza maelekezo ya Serikali kuhusu chanjo,kujikinga na UVIKO 19



Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma


MWENYEKITI wa Jumuiya ya Maridhiano Mchungaji Evance Chande amewaasa
wananchi kujenga desturi ya kufuata maelekezo ya Serikali kuhusu
chanjo ya UVIKO 19 na kufuata maelekezo yote ya kujikinga na kupunguza
maambukizi ya ugonjwa kama siyo kuyamaliza kabisa.


Akizungumza jijini hapa Mwenyekiti wa Jumuiya amesema kumekuwa na
tabia ya wananchi kusikiliza maneno ya watu wengine badala ya
kusikiliza Serikali inasema nini kuhusu kujikinga na maambukizi ya
UVIKO 19 na kusababisha maambukizi hayo kushamiri.


“Serikali imeleta chanjo kwa nia njema ,na imesema chanjo hiyo
inatolewa kwa mwananchi aliyemaa kwa hiyari yake wenyewqe kuchanja
,mimi sitaki kuamini kwamba serikali ina mpango wa kuwaangamizi
wananchi wake kwa kuwapa chanjo,hii ni dhana potofu.”amesema Mchungaji
Evance na kuongeza kuwa

“Tuache tafsiri potofu kwamba serikali inalazimisha watu kuchoma
chanjo ,hailazimishi hilo,kuchanja ni hiyari ,Rais Samia Suluhu Hassan
siku zote anasema mtu asilazimishwe bali aelimishwe kisha aamue mwenyewe
kuchanja ,lakini watu wamekuwa wakisikiliza mitandao na watu
mbalimbali wanaodai chanjo siyo salama ,hii siyo sawa,Mimi naamini
tutaweza kufanikiwa  kuondokana na janga la UVIKO 19 kama tutafuata
maelekezo ya Serikali.”

Aidha amewaasa viongozi wa dini zote waendelee kuelimisha wananchi
kuhusiana na kujikinga na ugonjwa huo kwa kufuata maelekezo
yanayotolewa na Serikali ikiwemo kutumia maji tiririka na
sabuni,kutumia vitakasa mikono na kuepuka mikusanyiko isiyokuwa ya
lazima.

“Viongozi wa dini tunao wajibu wa kuwaelimisha waumini wetu  kuhusu
chanjo,Mimi siamini kwamb Serikali ina nia ya kiwaangamiza watu wake
kupitia chanjo,hapan ,hilo siamini kama kuna serikali ya hivyo Duniani
kwani nguvu kazi ya Taifa ni watu na watu ndo sisi,sasa serikali iamue
kutuua wote halafu iweje ,hii ni tafsiri potofu ,hatupaswi kumsikiliza
kila mtu anayeongea,kila familia ina msemaji na msemaji wa Taifa la
Tanzania ni Rais Samia pamoja na viongozi wengine aliowapa ridhaa ya
kuzungumzia hilo “amesema na kuongeza kuwa

“Kwa mfano mimi hapa kanisani nimekuwa nikielimisha na Kuna wakati
tulisisitiza uvaaji wa barakoa na maji ya kunawa na
sabuni,ninchowaambia wananchi uviko unaua,sisi watanzania tunapaswa
tufuye maelekezo ya namna ya kujikinga hasa kiepusha mikusanyiko isiyo
ya lazima ,tuache salam za kupeana mikono na kukumbatiana

Ametumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi kuacha kulala kwenye misiba kwa kuangalia
ujirani Zaidi badala ya kuangalia afya zao huku akisema kwenye misiba
kunakuwa na mikusanyiko ambayo watu hukaa pamoja kwa muda mrefu.

“Kwenye misiba bado ni changamoto,watu wengi wanakusanyika na kulala
wengi kwenye chumba,hii ni hatari,kulala misibani tuache kwa ajili ya
tahadhari inasababisha maambukizi ,Serikali imeshazungumza tuchukue
tahadhari,tukizingatia haya Mungu atatutetea na maambukizi yataendela
kupungua ,ingawa hata Sasa Mungu ametutetea kwa kiwango kikubwa siyo
kama watu walivyodhani kwamba waafrika tutakufa kama kuku ,kama
alivyotutetea mwanzo bado ataendelea kututetea