January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti CHADEMA jimbo la Lindi,atimkia CCM

Na Penina Malundo, Timesmajira

MWENYEKITI wa Jimbo la Lindi kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ally Simba amejiunga na Chama cha Mapinduzi CCM baada ya kushawishika na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan anazofanya za kuleta maendeleo nchini.

Akizungumza baada ya kurudisha kadi ya Chadema Mkoani Lindi na kupokelewa na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mwenyekiti huyo amesema ameamua kurudi CCM A kutokqna na Rais Samia kufanya kazi za kuwaletea maendeleo wananchi.

Amesema miongoni mwa mambo yaliyomkosha yanayofanywa na Rais Samia ni katika maeneo matatu ikiwemo gesi Asilia ,Uboreshaji wa bandari ambapo zimepunguza msongamano kwa kiasi kikubwa bandarini na Kukuza Sekta ya Utalii kupitia Royal Tour.

“Nimeshawishiwa kwa muda mrefu ndugu,jamaa na marafiki ,hivyo nimeamua kurudi CCM kwani mama anafanya kazi na amenikosha katika maeneo mbalimbali.

“Nimekuwa CHADEMA kwa muda mrefu lakini baada ya kuona jitihada zangu haziwezi kufika mwisho nikiwa mpinzani nikaona niunge juhudi ,nihamie CCM nisaidiane na Mama Samia kwani anafanya kazi nzuri kwa kuwaletea maendeleo watanzania,”amesema.