December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti ACT-Wazalendo akutana na viongozi wa chama hicho taifa

Mwenyekiti wa Chama cha ACT – Wazalendo Taifa ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, Machi 08, 2024, amekukutana na kubadilishana mawazo na Wajumbe wa Sekretarieti ya Chama hicho ngazi ya Taifa makao makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam.

Kikao kilichoenda sambamba na kukagua jengo na ofisi yake mpya kama Mwenyekiti wa chama hicho ambaye ameambatana na Mke wake Zainab Kombo Shaib.

Ambapo Jumamosi ya Machi 09, 2024 Othman, atarejea na kupokelewa Visiwani Zanzibar, kwa mara ya kwanza akiwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa.