November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenezi aeleza mikakati ya CCM Bonyokwa

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Mwenezi wa chama cha Mapinduzi CCM kata ya Bonyokwa Bakari Ahmedy, ameeleza mikakati ya chama cha Mapinduzi CCM kata ya Bonyokwa kuhakikisha CCM wanakuwa na matawi ya ofisi Ili kurahisisha Shughuli za chama .

Akizungumza na waandishi wa habari Bonyokwa Wilayani Ilala Mwenezi wa CCM Bakari alisema kata ya Bonyokwa ni miongoni mwa kata 36 zinazounda matawi manne ambayo ni mkombozi ,Kinendile ,Kanada na Msingwa. .

“Mikakati ya chama CCM Bonyokwa tumejipanga kuhakikisha tunakuwa na Ofisi za matawi Ili kurahisisha shughuli za chama kila wakati na vikao vinafanyika ” alisema Bakari .

Mwenezi Bakari Ahmedy alisema Bonyokwa ni kata iliyotokana na kugawanywa kutoka Kata ya Kinyerezi miaka iliyopita hivyo ilikuwa na changamoto nyingi ambazo sasa zinafanyiwa kazi Moja wapo ni Ofisi za chama cha Mapinduzi .

Mwenezi Bakari alisema mikakati hiyo waliojiwekea kipaumbele cha kwanza kujenga Ofisi za chama kwa nguvu za Wananchi ni Ofisi tawi la mkombozi na Bonyokwa April 15 kuanza ujenzi .

Aidha alisema baada kumaliza kuanza ujenzi katika matawi mawili yatafuata matawi ya Kanada na tawi la CCM Msingwa lipo tayari ila litafanyiwa maboresho .

Alisema awali wana CCM wa Bonyokwa kilio chao kikubwa kilikuwa Ofisi ya Kata kwa sasa Ofisi imepatikana imefunguliwa rasmi sasa ni Wakati wa kutatua kero za chama na kufanya vikao vya chama .

Alisema wajumbe wa Kamati ya siasa na SECTRIET walikutana katika ofisi za chama kupanga vitu katika ofisi zao tayari kuanza kazi rasmi .

Wakati huo huo alisema CCM Bonyokwa imejipanga kuakikisha CCM inashika Dola katika chaguzi za Serikali za Mitaa mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 wa Wabunge Rais na madiwani.