December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

MWAUWASA yatunukiwa tuzo

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) imetunukiwa tuzo ya mshindi wa pili miongoni mwa Mamlaka za Maji nchini katika utoaji wa taarifa kwa wananchi.

MWAUWASA imetunukiwa tuzo hiyo jijini Dar-esSalaam Juni 22, 2024 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye wakati wa kikao kazi cha Maofisa Habari Serikalini.

Tuzo hiyo imepokelewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma MWAUWASA, Mohamed Saif.

Mbali na tuzo hiyo, MWAUWASA imepokea cheti cha kutambua jitihada za kipekee na mikakati bunifu ya mawasiliano inayotekeleza na ambayo imeleta mchango mkubwa katika Sekta ya Habari.

Kikao kazi hicho kimeshirikisha Maofisa Habari wa Serikali zaidi ya 500 kutoka Wizara, Taasisi, Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini.