Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA),imetekeleza agizo la
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew la kuwaunganishia wananchi wa Stone Town, Buswelu wilayani Ilemela huduma ya maji safi na salama.
Itakumbukwa Julai 27,2024,katika ziara yake ya nyumba kwa nyumba katika mtaa huo Mhandisi Kundo alimpa wiki mbili(siku 14), Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mwanza(MWAUWASA) Kanda ya Nyakato kuhakikisha wananchi wa mtaa wa Stone Town Kata ya Buswelu wanaunganishiwa huduma ya maji huku inakadiriwa wananchi zaidi ya 300 watanifaika.
Ambapo aliwaahidi wananchi wa mtaa huo pamoja na Meneja huyo wa MWAUWASA Kanda ya Nyakato kuwa Agosti 11,2024 atapita eneo hilo hili kuona kama agizo lake limetekelezwa.
Kaimu Meneja Kanda ya Nyakato kutoka MWAUWASA,Agnes William amesema alipewa kazi ya kukamilisha maunganisho mapya kwa wateja wa Stone Town na hadi sasa zoezi limekamilika na wateja wanapata huduma ya maji.
Agosti 11,2024 Mhandisi Kundo akiwa eneo hilo ameshuhudia nyumba kadhaa zikiwa tayari zimeunganishiwa huduma ya maji huku zoezi hilo likiendelea kutekelezwa na Mafundi wa MWAUWASA.
Mhandisi Kundo ameipongeza MWAUWASA kwa kutekeleza agizo hilo kwa wakati huku akiwaeleza wananchi kuwa licha ya kuunganishiwa huduma hiyo mamlaka hiyo itaendelea kutoa huduma kwa kutekeleza migao wakati miundombinu ya uzalishaji na usambazaji maji ikiendelea kuimarishwa.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maji kuendelea kutekeleza miradi ya kimkakati ili kuimarisha zaidi huduma ya maji kwa wakazi wa Mkoa wa Mwanza.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa eneo hilo wamepongeza kazi iliyofanyika na kutoa hamasa wa wananchi wengine kuendelea kuunga mkono jitihada hizo za Serikali kwa kutunza miundombinu ya maji na kulipa ankara (bili) za maji kwa wakati.
More Stories
SACP Katabazi: Elimu ya usafirishaji wa kemikali bado ni muhimu kwa watanzania
REA yajitosa kwenye nishati safi ya kupikia
Maghorofa Kariakoo mikononi mwa Tume