December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

MWAUWASA na mikakati ya kuboresha huduma ya maji Kangae’A’

Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza

Katika kukabiliana na changamoto ya upatikanaji maji eneo la Kangae’A’ Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza(MWAUWASA),ina mpango mkakati wa muda mfupi na kati wa kuboresha huduma hiyo kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA Neli Msuya wakati alipotembelea eneo la Kangae na kuzungumza na wananchi namna bora ya kuimarisha na kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji katika eneo hilo.

Ambapo amewaeleza wananchi wa eneo hilo kuhusu mipango ya muda mfupi na kati inayotekelezwa na MWAUWASA ili kuboresha huduma ya maji

Neli ameeleza kuwa mpango wa muda mfupi utakaotekelezwa eneo la Kangae ‘A’ ni uwekaji wa matenki ya lita 40,000 pamoja na kuimarisha mfumo wa usambazaji maji ili kukabiliana na changamoto ya maji katika eneo hilo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kangae ‘A’ Joseph Hondo ameishukuru MWAUWASA kwa kutembelea eneo hilo na kujadili kwa pamoja na wananchi namna ya kuimarisha hali ya upatikanaji maji.

Huku akiahidi kudumisha ushirikiano na wananchi wa Kangae katika utekelezaji wa miradi mingine.