Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC),Ndele Mwaselela, amesema chama hicho kwa Mkoa wa Mbeya kitashinda kwa kishindo,katika uchaguzi wa serikali za mitaa,unatarajia kufanyika Novemba 27,2024.
Mwaselela,amesema ushindi huo utapatikana,kwa sababu ni Mkoa pekee nchini hapa,unaosomeka duniani kupitia mtoto pekee Dkt.Tulia Ackson,ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge duniani.
Mwaselela amesema hayo Agosti 31,2024 wakati akizungumza na mama Lishe na Baba Lishe, kwenye mashindano ya mapishi yaliyoandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust,ilio chini ya Mkurugenzi wake Dkt.Tulia Ackson,ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Wanawake ni jeshi kubwa.Sina mashaka nikiona wanawake wakiungana kwa pamoja, nendeni mkawashauri jirani zenu, kuwa huyu dada anachapa mzigo ni kazi kuvaa viatu vyake.Nataka niwahakikishie kuwa Mbeya mjini ipo salama na Mkoa upo salama,”ameeleza Mwaselela.
Pia ameahidi kuongeza nguvu kwenye mfuko wa mama lishe,huku akieleza kuwa sadaka hiyo ataitoa kwa heshima ya Dkt.Tulia.
Sanjari na hayo,Mwaselela amesema kuwa pamoja na kazi wanazofanya mama lishe hao,pia amewaomba katika uchaguzi wakichague Chama Cha Mapinduzi.Pamoja na kuhakikisha Dkt.Samia Suluhu Hassan,anapata kura za kimbunga na kumlinda dada yake Dkt.Tulia.
“CCM,imejipanga kuleta wagombea wenye ushawishi,mama lishe nendeni mkachukue fomu, mgombee katika uchaguzi wa serikali za mitaa,ili mitaa iongozwe na wanawake na kata ziongozwe na Baba Lishe,nendeni mkafanye kazi msiogope chama kipo kitawalinda ,ninamwombea Dkt.Tulia na Rais Samia waendelee kufanya kazi kwa moyo kwa kugusa sekta mbalimbali,”amesema Mwaselela.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga,amewataka wanawake kujiamini katika uchaguzi mkuu ujao pamoja na serikali za mitaa.Sanjari na hayo amempongeza Dkt.Tulia kwa kuandaa mashindano hayo ambayo yamegusa mama lishe 1000 na baba lishe,kutoka kata 36 za Jiji la Mbeya yenye lengo la kuwainua kiuchumi.
Sophia Mwakagenda ni Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ),amesema kuwa nchi imetulia kwa sababu ya Rais Samia.Hivyo amewataka wanawake kutosubiri nafasi za viti maalum,badala yake waoneshe kuwa wanawake wanaweza kufanya Kazi.
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano