March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwaselela ataja sababu yeye kutogombea ubunge

Na Esther Macha,TimesMajiraOnline,Mbeya

MJUMBE wa Halmashauri Kuu Taifa (MNEC), Ndele Mwaselela ametoa sababu ya kutogombea nafasi ya  ubunge katika mchakato wa uchukuaji fomu  na urejeshwaji ulionza Juni 28 mpaka Julai 2,2025.

Mwaselela ametoa msimamo wake leo Jullai 3,2025 kwenye mkutano wake na waandishi wa habari katika ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM, Mkoa wa Mbeya .

Amesema kuwa kumekuwa na maneno mengi yakimhusisha kugombea ubunge Jimbo Fulani na kuwezesha watu jambo ambalo siyo kweli yeye hakuwa na lengo la kutia ya kuchukua fomu.

“Mimi nitaendelea kuwa MNEC kwani lengo langu ni kusaidia wananchi wangu awali nikiwa mdau wa maendeleo Mkoa wa Mbeya, nitaendelea kusaidia wananchi na hivi sasa nina programu nyingine ya  kuendelea kusaidia makundi mengine “Ndele Mwaselela amesema .

Katika hatua nyingine Mwaselela ameonya tabia ya baadhi ya watia nia kueleza kuwa wametumwa na uongozi wa juu jambo ambalo hata Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Rais Samia Suluhu Hassan amelikataza.

Mwaselela amesisitiza kuwa kila aliyetia nia ni maamuzi yake binafsi kugombea nafasi za ubunge,udiwani na kwamba kwa sasa ni watia nia na siyo wagombea mpaka yatakaporejeshwa majina matatu kwenye mchakato wa ndani wa chama.

“Nasisitia kwa sasa waliochukua fomu sio wagombea ni watia  tusubiri wakati wa kurejeshewa majina matatu ,watakapoanza kujitambulisha kwa wananchi tutawaita wagombea rasmi,”amesema  Mwaselela.

Aidha Mwaselela amesema katika nafasi yake ya MNEC anahitaji kutumikia wananchi  zaidi na kubanisha hata awali alikuwa akifanya hivyo na hatokuwa tayari kurukaruka .

Awali,Katibu wa CCM ,Wiyala ya Chunya Charles Jockel ,ameonya watia nia kuacha kuchafuana kabla ya majina yao kurejeshewa kwenye kura za maoni.

Jockel ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna walivyojipanga kukabiliana na Hali hiyo.