Na Neema Mtunguja, TUDARCo
TIMU za mpira wa kikapu za wasichana na wavulana kutoka jijini Mwanza zimeendelea kutikisa kwenye michuano ya UMISSETA inayoendelea mjini Mtwara.
Katika mechi zilizochezwa jana, timu ya wavulana ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa vikapu 66-15 dhidi ya Kigoma huku ile ya wasichana ikiwachana Iringa vikapu 87-6.
Ushindani mkali uliopo baina ya timu za Mikoa mbalimbali inayoshiriki katika mashindano hayo yanayoendelea katika viwanja mbalimbali vya Chuo cha Ualimu Mtwara umekuwa kivutio kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia vipaji vya watoto wao.
Karibu michezo yote imekuwa ikivuta hisia za wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia michezoni hiyo hususani mpira wa miguu, na katika siku tatu za kwanza kivutio kingine ni mchezo huo wa kikapu (Basketball) na Mpira wa wavu (Volleyball).
Mbali na Mwanza, timu ya wavulana ya Tanga imewachapa Geita vikapu 45-5, Pwani imewafunga Ruvuma 46-18 wakati wenyeji Mtwara wakikubali kichapo cha vikapu 47-11 kutoka kwa Kilimanjaro huku kwa upande wa wasichana Shinyanga I mewachapa Mtwara 20-0 na Geita wakiichapa Lindi 27-19.
Mabingwa watetezi Mtwara, wamekuwa na sifa ya kipekee ya kuwa na timu bora ya mpira wa wavu baada ya kuwafunga Tabora seti 3-2, Kagera imefungwa na Mbeya seti 3-0, Mara imewafunga Pemba seti 3-0 huku kwa upande wa wasichana Tanga imeifunga Kigoma seti 3-0.
Katika mchezo wa Netiboli Mara imeifunga Arusha magoli 32-19, Manyara imefungwa na Pwani 20-31, Dar es salaam imeifunga Ruvuma magoli 37-9, Geita imefungwa na Songwe 18-32, Mtwara nayo imefungwa na Rukwa 15-34 na Unguja imekung’utwa na Singida magoli 12-29.
Katika mpira wa soka wasichana, Manyara imeibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya songwe, Mara imeifunga Mtwara 3-0, Ruvuma imetoka sare ya goli 3-3 na Rukwa wakati Mwanza imeifunga Tabora 1-0.
Mpira wa mikono wavulana, Lindi imeifunga Simiyu magoli 19-16, Mara imeifunga Dar es salaam 23-17, Singida imefungwa na Unguja magoli 11-37, Tabora imeichabanga Kigoma magoli 24-8 huku kwa upande wa wasichana Singida imefungwa na Tabora 5-14, Songwe imeichalaza Dodoma magoli 26-4, Rukwa imefungwa na Mbeya magoli 9-24, na Dar es salaam imeifunga Mara 17-11.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania