Na Joce Kasiki, TimesMajira, Online,Dodoma
MBUNGE wa Njombe kwa tiketi ya CCM, Deo Mwanyika, amesema Wizara ya Madini inapaswa kutenga fedha kwa ajili kufanya utafiti ili kujua sekta ya madini nchini inakua kwa kiasi gani, huku akisema suala hilo litaleta tija katika seta hiyo.
Mbunge huyo ameasemwa hayo wiki iliyopita alipokuwa akichangia bungeni, jijini Dodoma.
Amesema kama kutakuwepo na bajeti ya utafiti itasaidia sekta hiyo kuchangia zaidi katika pato la Taifa.
“Sekta ya utafiti imepungua sana ama fedha hiyo haipo kabisa,hata katika bajeti yake waziri hajaongelea kabisa suala hilo, ingekuwa vyema utafiti ufanyike kwa fedha zetu ili itupe nguvu ya kujua sekta inakua kwa ukubwa gani na kwa miaka mingapi,”amesema Mwanyika na kuongeza;
“Baada ya mageuzi makubwa katika sekta ya madini tumeshuhudia mchango wa sekta ya madini na kukua kwake kumeongezeka kwa kiasi kikubwa.”
Amesema kwa sasa sekta ya madini inachangia asilimia 5.2 kwenye pato la Taifa na inaleta matumaini kwamba mchango wa sekta hiyo utaendelea kuongezeka zaidi.
Ameongeza kuwa aisha ya sekta ya madini yanategemea sana utafiti, huku akisema kuendelea kukua na kuongezeka kwa mchango wa sekta hii zaidi kunahitaji kazi ya ziada.
Aidha ameshauri wizara hiyo kuangalia na madini mengine ili yaweze kuchangia pato la Taifa badala ya kutegemea dhahabu pekee.
“Bado sekta hii kwa kiasi kikubwa inategemea dhahabu pekee,lakini Dhahabu ina tabia ya kupanda bei na kushuka,sasa ni wakati muafaka kwa Serikali kuangalia na madini mengine ili yaweze kuchangia vyema katika pato la Taifa,”amesema Mwanyika.
Hata hivyo tumeshuhudia sekta hii kukua, lakini haiongezi uzalishaji kwa maana ya migodi mipya.
Ameomba wizara hiyo kuangalia upya na kurekebisha sheria za sekta ya madini ili iweze kuchangia kwa kiasi kikubwa zaidi.
Katika mwaka wa fedha wa 2021/22 Wizara ya Madini imeomba kiasi cha sh. bilioni 66.8 ili iweze kutekeleza majukumu yake katika kipindi hicho.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote