Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari tarehe 13 Machi, 2026 ameapishwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, katika hafla fupi ya uapisho iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Jijini Dodoma.
Johari ameapa mbele ya Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania,George Masaju, kufuatia kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume hiyo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameteuliwa kuwa mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kufuatia kuteuliwa kwake kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa mara ya pili na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Novemba, 2026.

Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameapishwa kuwa Kamishna kutimiza takwa la Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Na. 4 Sura ya 237 inayomtaka kila Kamishna kuapishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yake.
Sambamba na Johari, Wajumbe wengine wa Tume ya Utumishi wa Mahakama walioapishwa ni pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufaa Gerson Mdemu, na Mawakili wa Kujitegemea Thomas Nyanduga na Dorcas Mutabuzi.

More Stories
NMB ilivyosaidia Serikali kukusanya zaidi ya Sh trilioni 9.8
Serikali yaongeza nguvu kwa wachimbaji wadogo,yasisitiza usalama Migodini
REA imeleta mageuzi sekta ya nishati