Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Mwanasheria Hamza S. Johari ameshiriki zoezi la upigaji wa kura,katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika nchi nzima 27 Novemba mwaka huu,ambapo amepiga kura Kata ya Ipagala,kituo cha Mbuyuni, Ilazo jijini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya kupiga kura Mwanasheria Mkuu wa Serikali amefurahishwa na kuridhishwa na mazingira ya kituo hicho na zoezi zima la upigaji wa kura lilivyoendeshwa, ambapo amesema utaratibu wa upigaji wa kura umekuwa rahisi, na huku akiwasifu wasimamizi wa uchaguzi huo kwa kutoa maelekezo vizuri kwa wapiga kura.
“Utaratibu safari hii umeboreshwa, hata utoaji wa elimu kabla ya kupiga kura umeweka vizuri,”.
Zoezi la upigaji wa kura kuwachagua Viongozi wa Serikali za Mitaa,limefanyika nchi nzima ambapo wananchi wamejitokeza kwenye maeneo mbalimbali kutekeleza haki yao ya msingi kikatiba ya kuwachagua Viongozi wao wa mitaa,vijiji na vitongoji.
More Stories
CHADEMA yasikitishwa mawakala wao kuzuiliwa
Rais Samia amlilia Dkt. Ndugulile
Makada wa CHADEMA,mbaroni kwa tuhuma za kukimbia na karatasi za kuraÂ