Judith Ferdinand, Timesmajira Online,Mwanza
Watu watano akiwemo mwanafunzi wa kidato cha pili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya vikongwe wawili yaliotokea wilayani Sengerema mkoani Mwanza mwaka jana.
Ambao wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya Sophia Maduka,(61) na Mathias Lusesa,(73) wote wakulima na wakazi wa Lwenge Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
Akizungumza mkoani hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa ameeleza kuwa mnamo Oktoba 12,2023 majira ya saa mbili (20:00) usiku katika Kijiji cha Lwenge Kata ya Kagunga Wilaya ya Sengerema watu wawili waliuawa kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali sehemu mbalimbali za miili yao.
Mutafungwa ameeleza kuwa baada ya taarifa hiyo kuripotiwa kituo cha polisi,jeshi hilo lilifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao waliokuwa wamejificha kukwepa mkono wa sheria.
Ambapo Januari 06,2024 kwa nyakati tofauti na maeneo tofauti katika Mkoa wa Geita na Shinyanga Askari wa upelelezi kutoka Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Askari wa mikoa hiyo jirani walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao watano.
Mutafungwa amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Selina Mchele(48),mkulima na mkazi wa Kijiji cha Mwakilemwa,Maneno Mashauri,(19)mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Lwenge Wilaya ya Sengerema, Majaliwa Damas,(22) Mganga wa tiba asilia,mkazi wa Masumbwe mkoani Geita, Ntingwa Kilimanjaro kwa jina maarufu Shetani(42)mkulima na mkazi wa Kijiji cha Mbamba mkoani Geita na Emmanuel Damas,(34),Mganga wa tiba asilia,mkazi wa Kijiji cha Burungwa mkoani Shinyanga.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â