Na Moses Ng’wat, Timesmajira Online,Mbozi
Jeshi la Polisi mkoani Songwe linamshikilia Lukia Magwaza (21), Mkazi wa kijiji cha Shasya Kata ya Halunga, Wilayani Mbozi kwa tuhuma za kumuoa mwanafunzi (jina limehifadhiwa) aliyetakiwa kujiunga na kidato cha tano.
Mwanafunzi huyo ambaye naye anashikiliwa na jeshi hilo anadaiwa kuwa alimaliza kidato cha nne mwaka 2022 katika shule ya sekondari ya Spring Valley iliyopo mkoani Iringa na alitakiwa kujiunga na kidato cha tano baada ya kupata ufaulu wa daraa la tatu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya, amewaambia waandishi wa habari kuwa, mtuhumiwa huyo alikamatwa usiku wa Julai 16,2023 kwa ushirikiano kati ya jeshi hilo na uongozi wa kata.
Hata hivyo, Kamanda Mallya amesema wanamshikilia mwanafunzi huyo kwa uchunguzi zaidi kwani baada ya kuhojiwa alidai kuwa hajui kama alichaguliwa kuedelea na masomo kwa kujiunga na kidato cha tano.
“Mtuhumiwa na mwanafunzi wote wamekamatwa wapo kituoni kwa mahojiano zaidi, kwani mwanafunzi anadai kuwa alimaliza kidato cha nne na kufaulu kwa kupata daraja la tatu, lakini mpaka sasa alikuwa hajui kama alichaguliwa kujiunga na kidato cha tano” alifafanua zaidi Kamanda Mallya.
Aidha, Kamanda Mallya ameongeza kuwa Jeshi hilo linaendelea kuwatafuta wazazi wa pande zote mbili ambao wametoroka wanaodaiwa kushiriki kupanga ndoa hiyo.
“Kuna mazingira ambayo yanaonesha kuwa wazazi wa pande zote mbili walibariki mpango wa ndoa hiyo na baada ya kujua kuwa vyombo vya dola vimebaini wameamua kutorokea kusikojulikana,” amesema Kamanda Mallya.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi