Na Moses Ng’wat, TimesMajira Online, Mbozi.
POLISI MKoa wa Songwe limemkamata Amiza Nzunda (26) makzi wa Lutumbi katika mji wa Mlowo Wilayani Mbozi ambaye ni mama wa kambo akihusishwa na kifo chenye utata cha mwanae wa kufikia Nathan Sikalengo (7).
Marehemu ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Lutumbi Wilayani humo anadaiwa kufariki baada ya kuanguka ghafla na kuanza kutoka mapovu mdomoni na damu puani akiwa na mama yake huyo wa kambo ndani ya nyumba yao.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya aliwaambia waandishi wa habari kuwa tukio Hilo lilitokea Juni 5 2023, majira ya saa 2:00 usiku.
Kamanda Mallya alisema jeshi Hilo linaendelea na uchunguzi na wanamshikiliwa mama wa kambo wa mwanafunzi huyo kwa mahojiano zaidi, huku sampuri za mapovu zikichukuliwa kwa ajili ya vipimo vitakavyosaidia kwenye u chunguzi wa kifo hicho.
“Tunaendelea kumshikilia mama wa kambo kwa mahojiano zaidi kwani tumepokea taarifa kutoka kwa majirani kwamba mtuhumiwa alikuwa akimfanyia marehemu vitendendo vya kikatili na manyanyaso” alisema Kamanda Mallya.
Akifafanua zaidi kamanda Mallya alisema kabla ya tukio Hilo, mama huyo wa kambo wa marehemu alishawahi kufikiishwa katika dawati la jinsia akituhumiwa kwa manyanyaso.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbozi,Dk.Keneth Lesilwa alikiri Hospitali hiyo kupokea mwili wa mwanafunzi huyo na kwamba sampuli zimechukuliwa na kupelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali.
Naye Katibu wa Mtaa wa Lutumbi mjini Mlowo ,Anyimike Msongole alisema walipokea taarifa za kifo cha mwanafunzi huyo kutoka kwa majirani na baada ya kufika eneo la tukio walikuta marehemu akiwa tayari amefariki huku akiwa ametokwa na mapovu mdomoni na damu puani.
“Sisi kama viongozi baada ya kuona hali hiyo tulitoa taarifa polisi, lakini tayari wananchi walishajipanga kumshambulia mama wa kambo na marehemu wakimhusisha na kifo hicho” alisema Msongole
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano