Judith Ferdinand,Timesmajira Online,Mwanza
Mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Luchelele wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, Kurwa Mkami(9),amepoteza maisha baada ya kushambuliwa na mamba,wakati akioga kwenye fukwe za Ziwa Victoria.
Kamanda wa Polisi DCP.Wilbrod Mutafungwa,akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa,Novemba 8,2024,amesema tukio hilo lilitokea Novemba 5,mwaka huu majira ya saa 12,jioni katika mwalo wa Ihumilo kwenye fukwe za Ziwa Victoria Kata ya Luchelele wilayani Nyamagana,ambapo marehemu Kurwa wakati anaoga kwenye fukwe hizo alishambuliwa na kisha kuvutwa kwenye maji na mamba.
DCP.Mutafungwa,ameeleza kuwa baada ya taarifa hizo kuripotiwa kwenye kituo cha Polisi,Jeshi hilo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Wanyama Pori(TAWA) na wananchi wa eneo hilo,walifika katika mwalo huo na kuanza jitihada za kumtafuta Kurwa.
“Ilipofika Novemba 7,2024,tulifanikiwa kuupata mwili wake ukiwa na majeraha ya kujeruhiwa na mamba sehemu mbalimbali,Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitaalam na kukabidhiwa ndugu kwa taratibu za mazishi,”.
Jeshi hilo pamoja na kutoa elimu pia linawaasa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya fukwe za Ziwa Victoria,kuchukua tahadhari za kiusalama wakati wanafanya shughuli zao kwenye fukwe za ziwa hilo ili kuepuka kushambuliwa na wanyamawakali
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba