December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwanafunzi adaiwa kuuwawa na rafiki wa baba yake

Judith Ferdinand,Timesmajira Online,Mwanza

Tatu Hamis Daniel(9),mwanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi Nabweko,mkazi wa kijiji cha Nabweko wilayani Ukerewe mkoani Mwanza,amedaiwa kuuwawa kwa kukabwa shingoni kisha kubakwa,na mtuhumiwa ambaye ni rafiki wa baba yake marehemu.

Ambapo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamsaka mtuhumiwa wa mauaji hayo aliyejulikana kwa jina moja la Jackson,ambaye ni kuli na mkazi wa Nansio,wilayani Ukerewe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,DCP.Wilbrod Mutafungwa,akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa,Novemba 8,2024,amesema,Novemba 4,mwaka huu,majira ya saa 12 na nusu jioni, kijiji cha Nabweko,Wilaya ya Ukerewe,ulionekana mwili umetelekezwa kwenye jengo ambalo halijakamilika kujengwa.Mwili huo uliotambuliwa na wazazi wa marehemu,ambao ni Hamis Daniel(39) na Rehema Peter(43),wote wakazi wa Nabweko kisiwa cha Irugwa,kuwa aliyeuwawa ni mtoto wao.

DCP.Mutafungwa,amedai kuwa ,Novemba 3,2024,majira ya saa mbili usiku,marehemu(Tatu),alikuwa anacheza na wenzake,ndipo alipotokea mtuhumiwa(Jackson),kwa jina maarufu Mjomba,amabye ni rafiki wa baba wa marehemu ,akamchukua kwa ahadi ya kwenda kumnunulia pipi dukani.

Lakini alitoweka nae kusikojulikana hadi Novemba 4,2024,Tatu alipopatikana akiwa ameishafariki.Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitaalamu na kukabidhiwa ndugu kwa ajili ya mazishi.

“Wananchi tushirikiane,kwa kutoa taarifa itakayofanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo,popote alipo ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake,”.