January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwalimu mbaroni akituhumiwa kwa unyang’anyi kwa silaha

Na Esther Macha, TimesmajiraOnline,Mbeya

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu watatu akiwemo Mwalimu wa shule ya msingi Mwaselela, Azimio Gerald (31),Mkazi wa ZZK Mji mdogo wa Mbalizi kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha,uporaji pamoja na uvunjaji wa nyumba.

Watu wengine wanaohusika katika tukio hilo ni, Furaha Issa ,(32) na Goodluck Mwakajisi (25) wote wakazi wa Iwambi.

Akizungumza na waandishi wa habari Januari 26, mwaka huu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi, Benjamin Kuzaga amesema kuwa watuhumiwabhso walikamatwa Januari 25 mwaka huu katika misako iliyofanyika maeneo mbalimbali ya Mji mdogo wa Mbalizi.

Aidha Kamanda Kuzaga ametaja baadhi ya mali za wizi walizokutwa nazo watuhumiwa hao ni television 2, redio subwoofer 3, redio ndogo 4 na spika zake, laptop 8, simu za mkononi 16 pamoja na mashine moja ya kupimia damu.

Ameongeza kuwa, watuhumiwa wamrkutwa na vifaa mbalimbali vya kuvunjia nyumba na maduka, visu 4, mapanga 3 huku baadhi ya mali zimetambuliwa na waathirika wa uhalifu huo.

Jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi kufika kituo cha Polisi Mbalizi kwa ajili ya kutambua mali zao.