November 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwakibete :Wanafunzi wanatakiwa kuwa wabunifu wanapomaliza masomo yao

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete amewataka wanafunzi kuwa wabunifu na kusoma kwa bidii ili wanapomaliza masomo yao waweze kuwa na maarifa na ujuzi wa kutoka wa kujiajili na kuajiliwa.

Mwakibete amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa mahafali ya 38 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), ambapo wanafunzi 2,771 walihitimu masomo yao kwa kozi mbalimbali.

Amewata wanafunzi wanaendelea na mafunzo wawe wabunifu kwa kuzingatia uchumi wa kisasa unahitaji nguvu kazi zenye maarifa na ujuzi wa juu zaidi ili kuendana na soko la dunia.

“Wanafunzi mnaobaki katika zama hizi ambazo kuna mabadiliko makubwa ya teknolojia ni dhahili kwamba ubunifu ni jambo muhimu kwa nchi yetu katika kujenga uchumi imara kwa hiyo ni rai yangu kwenu mjitume katika masomo yenu,” amesema Mwakibete 

Pia, aliwataka wahitimu hao wasiridhike na utaalamu  waliyoupata, endeleeni kutafuta utaalamu wa juu zaidi ili Taifa liwe na wataalam wa kutosha na wenye sifa zote zinazohitajika kwenye sekta ya uchukuzi na usafirishaji.

“Ninatambua kuwa tuzo mtakayoipata leo ni msingi kwenu katika safari ndefu na kuwa na hazina kubwa ya rasilimali watu inayotegemewa sana na Taifa hususan katika ya chukuzi na usafirishaji,”amesema 

Pia, Naibu huyo alitoa wito kwa chuo hicho kuwa vifaa ambavyo Serikali imevinunua kwa gharama kubwa kwa ajili ya mafunzo hapa chuoni vitunzwe ili watanzania wengi wanufaika katika kupata mafunzo haya.

“Serikali inafanya haya yote ili NIT itoe elimu bora ili kiandae wataalam wa kutosha wenye ujuzi kwa.ajili ya sekta ya uchukuzi na usafirishaji,” amesema

Akizungumzia suala kuajili wazawa, alimuhakikishia Mkuu wa chuo hicho, Profesa Zacharia Mganilwa kuwa katika miradi inayoendelea na itakayofuata, ambapo Serikali imewekeza zaidi ya trilioni 16 kwenye ujenzi wa Reli ya kisasa wazawa watapewa kipaumbele.

Amesema kuwa kwenye mikataba wanayoingia sasa hivi na wakandarasi, kipengele cha kuajili wazawa kipo kwa asilimia isiyopungua 50 ambapo inatengwa Dola za Marekani milioni 200 zitumike kwa ajili ya ‘Local content’

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa chuo hicho, aliishukuru Serikali kwa kuwapatia maeneo ya viwanja vya ndege vya Kitaifa Mwalimu Julius Nyerere na uwanja wa Kilimanjaro kwa ajili ya mafunzo ya usafiri wa anga.

Naye, Mkuu wa chuo hicho, Profesa Mganilwa amesema kuwa huu ni muda mwafaka kwa Wizara mama kuwatumia wataalam wa ndani kwa sababu zinatumika fedha nyingi sana kwa ajili ya kuwasomesha.

“Katika miradi hii hata kama italeta mtaalamu kutoka nje ya nchi wekeni kipengele cha mikataba yao kuwe na local content tuwe na mtaalam pia kutoka ndani  nchi itasaidia sana,”

“Kwa sababu mara nyingi nimeudhulia vikao vingi wataalam wanapokuwa wamekuja kufanya stadi mimi na kwenda na wataalam wangu mkianza kuuliza maswali yenye Taifa ndani yake mara nyingi wamekuwa wakali na wengine ndiyo wanatoka nje kuvuta sigara,” amesema Profesa Mganilwa