Esther Macha, Timesmajira Online,Mbeya
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mchungaji Jacob Mwakasole amesema matarajio yake ni kuona maono ya Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo ni kuwa na misingi ya umoja wa kitaifa, ustawi wa jamii na msukumo wa maendeleo yanatimia.
Mchungaji Mwakasole amesema hayo leo katika ofisi za chama hicho mara baada ya kurejesha fomu ya kuwania nafasi Uenyekiti CCM Mkoa .
Amesema kiu yake ni kuona matarajio ya Rais.Dkt Samia yanatimia ikiwa ni pamoja na kukijenga chama na kupata ushindi wa kishindo 2025 pamoja na uchaguzi wa serikali za mitaa utakaojumuisha wenyeviti wa vijiji na vitongoji.
Mchungaji Mwakasole amesema kuwa nia na madhumuni yake ni kutaka kuimarisha siasa Mkoa wa Mbeya ili iweze kushamili zaidi kwa sababu chama hicho mkoani humo kimekuwa na msukumo mkubwa na mvuto.
“Kazi yangu ni kuwaunganisha wanachama wetu kujiandaa na uchaguzi ujao wa wenyeviti wa serikali za mitaa,vitongoji na vijiji,lakini pia uchaguzi wa mwaka 2025 kumpata Rais wetu na hii ndo imenisukuma kuomba nafasi hii tena ili niwaongoze wenzangu,”amesema Mchungaji Mwakasole.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Clemence Mponzi amesema kuwa zoezi hilo lilianza Novemba 12 mpaka Novemba 16 mwaka huu na kuwa mpaka sasa waliochukua fomu ni 23 na kusema huku wanawake ni watatu.
Wakati huo huo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyanava amekuchukua fomu ya kuwania kiti hicho .
Lyanava amesema kuwa ameamua kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Uenyekiti kwa mujibu wa Katiba ili kushirikiana na wenzake kuhakikisha anakijenga chama kwa kushirikiana na wanachama wa chama kwa kuingiza wanachama wengi na kuhakikisha CCM inaendelea kushika dola.
More Stories
Kamati ya Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini yagawa vifaa vya ujenzi
Hatma mrithi wa Kinana kupatikana
Mrithi wa Kinana CCM kujulikana katika Mkutano Mkuu wa Jan 18/19