Na Omary Mngindo, TimesMajita Online, Mlandizi
MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoani Pwani, Michael Mwakamo amesema yupo mbioni kukutana na viongozi wa Vyama vya Mpira wa miguu na cha waamuzi ili kuandaa mafunzo ya awali kwa vijana chini ya miaka 17.
Mafunzo hayo ya ukocha na uamuzi wa mpira wa miguu yanalenga kuwapatia uelewa zaidi wa kisheria vijana wanaoshiriki mchezo huo, ili washiriki wakitambua miongozo yote tofauti na ilivyo sasa.
Mwakamo ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na Bodi inayosimamia michuano ya Mwakamo Cup aliyoianzisha kwa lengo ka kuibua vipaji vya vijana ambao wataweza kujiajiri kupitia sekta hiyo ya michezo.
Alisema, kwa hapa nchini na duniani kote mchezo huo ndio unaoongoza kwa lakini vijana wengi wanashiriki pasipo kupata mafunzo sahihi yanayouongoza hivyo kuwepo kwa mafunzo hayo kutawaongezea uelewa zaidi.
“Mwezi ujao michuano ya Mwakamo Cup itaendelea katika hatua ya Jimbo, baada ya kukamilika hatua ya awali iliyofanikisha kuundwa kwa kombaini za Kata, ambazo zitacheza hatua inayofuata ya Ligi ya Mbunge ngazi ya Jimbo mwezi Julia,” alisema Mwakamo.
Amesema, baada ya kukamilika kwa hatua ya Jimbo na kupatikana kwa bingwa wa Mwakamo Cup, atazungumza na viongozi wa Chama cha soka pamoja na cha waamuzi kuona ni namna gani watakavyoweza kuandaa kozi kwa vijana hao.
“Kwa kuwa huu ni mwaka wangu wa kwanza kwa ubunge, nitaanza na vijana wachache wanaoshiriki mchezo huo kwa maana ya makocha na waamuzi, malengo yangu ni kuwapatia ujuzi zaidi tofauti na sasa ambapo wanashiriki pasipokuwa na elimu hiyo,” amesema Mwakamo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Mwakamo Cup, Nassoro Mbilinyi amesema kuwa, hatua ya Mbunge huyo ya kuandaa mafunzo hayo yanalenga kuwakomboa vijana na kwamba itawatengenezea fursa ya ajira kupitia mchezo huo.
“Binafsi Mwakamo namuona ni kiongozi mwenye malengo ya kuwakomboa wana-Kibaha Vijijini katika sekta mbalimbali, kuandaa kwa kozi za ukocha na uamuzi unalenga kuona mchezo unachezwa ukizingatia sheria na taratibu zote tofauti na sasa,” amesema Mbilinyi.
Pia itaiwezesha Halmashauri ya Kibaha (Kibaha Vijijini) kuwa na makocha na waamuzi wenye taaluma hivyo kuviwezesha vilabu kuwa katika viwango bora hivyo kushiriki michuano mbalimbali wachezaji kuitambua zaidi.
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025