Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
RAIS wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)Wakili, Boniface Mwabukusi amesema kuwa chama hicho kufanyakazi kwa kushirikiana na serikali siyo kulamba asali kama wanavyosema wananchi bali kipo kwajili ya kusaidia jamii.
Mwabukusi ametoa kauli hiyo jijini hapa leo Februari 3,2025 katika viwanja vya Chinangali alipokuwa akitoa taarifa yake mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hasani wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya Sheria yenye kauli mbiu isemayo “Tanzania ya 2050 Nasafi ya taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya dira ya Taifa ya Maendeleo”
Amesema kuwa chama hicho kipo kwajili ya kusaidia jamii kupata haki bila upendeleo wa aina yeyote.
Kuonya,kukemea,kushauri na kupongeza kama itabidi kwa ajili ya manufaa makubwa ya nchi na siyo chama cha siasa na chama hicho hakifanyi biashara bali kuitetea jamii.
Aidha Mwabukusi ameishukuru Wizara ya Katiba na sheria kuwatupatia gari na kueleza kuwa gari hiyo itatumiwa kwa ajili ya kufanya kazi ya kutafuta haki kwa watu ambao wanahitaji msaada wa kitaifa.
“Unakuta mtu analalamika TLS kupewa gari,TLS haipokei Rushwa ni chama ambacho kinasimamia sheria na hakipo kwa ajili ya kufanya utabiri wala kufurahisha watu wa upande mmoja na kukandamiza upande mwingine bali sheria inasimawa kwa watu wote,”amesema Mwabukusi.
Amesema TLS haipokei Rushwa licha ya kuwa zipo changamoto mbalimbali ambazo wanakabiliana nazo ikiwa ni pamoja na vijana wengi ambao ni mawakili wanakumbana na suala la kikodi ambazo zinawakatisha tamaa na kushindwa kufanya kazi zao kwa ufasaha.
Hata hivyo Mwabukusi amesema kuwa pamoja na serikali kuboresha miundombinu ya kimahakama lakini bado kuna haja kubwa ya kuboresha masilahi ya watumishi wa Mahakama hususani Mawakili na Majaji kwani hao wanawahudumia wananchi kwa ukaribu zaidi.
“Ni ngumu Hakimu,Mwanasheria kumuhudumia mwananchi akiwa na msongo wa mawazo(Stress) na anayetafuta haki ni mwananchi ambaye anatafuta haki hivyo ni bora kuboresha masilahi ya mawakili na mahakimu”ameeleza Mwabukusi.
Katika hatua nyingine Mwabukusi ameitaka serikali kuona uwezekano wa kuifanya Taasisi ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kuwa na meno ili kuweza kufuatilia masuala ya watu wanaopotea,kutekwa,kurejeshwa na watu kuuliwa na wakati mwingine hata pale ambapo panaonekana kutofikiwa kwa kufanya uchunguzi panafikika.
Akizungumzia juu ya vitendea kazi amesema kuwa TLS bado haina vitendea kazi vya kutosha na kwa maana hiyo inafungua milango na madirisha kwa mtu yoyote anayetaka kuwasaidia awasaidie lakini wakitambua kuwa hiyo siyo sehemu ya rushwa bali ni kwa ajili ya kurahisisha ufanyaji wa utetezi kwa Umma na jamii kwa ujumla wake.
Hata hivyo Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake katika maadhimisho hayo amemjibu Wakili huyo kuwa maombi yao yamepokelewa
ambapo amesema yalikuja katika wakati bajeti imeshapangwa hivyo itashughulikiwa mwaka huu wa fedha 2025/26.
Akijibu suala la mgogoro wa kisheria Rais Dkt.Samia amesema amelipokea na kuitaka Wizara ya katiba na Sheria kushughulikia suala hilo
Suala na kuimarisha teknolojia na vifurushi Rais Samia amesema watakaa na Makampuni kuangalia namna ya kutoa ruzuku na kuona jinsi watakavyoweza kufanyakazi .
“Kuhusu mafunzo ya mara kwa mara ya kwa Mahakimu na Mawakili hili nimelipokea na
Mawakaili wanapoenda kusimamia kesi hapa ni elimu ya sheria na hii siyo kwa wananchi hata ndani ya serikali tunatakiwa kupata elimu,
“Kuhusu mfuko wa taasisi natambua katika malipo ya ada kuna fedha inaingizwa milioni 344 imeingizwa katika mfuko huo lakini tumejadili na Jaji Mkuu tuone namna ya kuongez,”amesema Rais Samia.
More Stories
Miaka 48 ya CCM,wanachama kutambulishwa wagombea Urais
Waislamu wamuombea dua Rais Samia,wasisitiza umoja
Samia: Serikali imejifunza somo kuporomoka ghorofa