January 4, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mvua ya upepo yasababisha maafa Rukwa

Na Israel Mwaisaka, TimesMajira Online, Kalambo

JUMLA ya watu 150 wamebaki bila makazi baada ya nyumba 30 kuezuliwa paa na nyingine zimebomoka kufuatia mvua kubwa iliyonyesha juzi katika Kijiji cha Kaluko kata ya Chitete wilayani Kalambo mkoani Rukwa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Edwin Kasama amesema kuwa mvua hiyo ilianza kunyesha Siku ya Octoba 26 majira ya saa 10 jioni zikiwa zimeambatana na upepo mkali.

Amesema kuwa ulianza upepo mkali Kisha ikafuatia mvua kubwa ambapo ilisababisha kubomoka baadhi ya nyumba kijijini hapo huku nyumba nyingine zikiezuliwa mapaa na kuziacha baadhi ya familia bila nyumba za kuishi.

“Baadhi ya wanakijiji nyumba zao zimebomoka kabisa hawana hata sehemu ya kulala tena wana watoto hivyo tunaiomba serikali iwasaidie kwakua wanapitia wakati mgumu kwakua vitu vyao vimeharibika kabisa” alisema Kasama.

Mmoja wa wakazi wa Kijiji hicho Paskalia Katata amesema kuwa tukio hilo limewaacha katika hali mbaya kwani hawana fedha za kukarabati nyumba zao zilizoharibika wanategemea tu msaada wa wahisani na serikali kwakua hali zao ki-uchumi siyo nzuri.

Naye diwani wa Kata ya Chitete, Patrick Benson amesema kuwa kutokana na tukio hilo baadhi ya wananchi ambao nyumba zao zilisalimika wamejitolea kwa kuzipa hifadhi familia ambazo makazi yao yalibomoka katika tukio hilo.

Amesema kuwa changamoto iliyopo ni namna ya kuwahudumia wananchi ambao walikumbwa na mkasa huo kwani hawana chakula pamoja na mahitaji mengine muhimu kwakua vitu walivyokuwa navyo viliharibika baada ya kulowana na mvua.

Mkuu wa wilaya ya Kalambo Lazaro Komba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanajenga nyumba bora zitakazo himili pindi panapotokea mvua zenye upepo mkali na majanga mengine.

HiMwisho
PICHA
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Razaro Komba
Na Israel Mwaisaka,
Kalambo