Na Mwandishi Wetu, timesmajira
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Anderson Mutatembwa amemtaka Mkandarasi anayejenga Jengo Jipya la Wizara hiyo lililopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma kuongeza kasi ili Jengo hilo liweze kukamilika kwa wakati uliopangwa
Ametoa wito huo leo Machi 9, 2023 wakati alipotembelea katika Jengo hilo kwa lengo la kujionea hatua ilipofikia ambapo Mutatebwa amesema kukamilika kwa Jengo hilo kutasaidia Wizara kuweza kutoa huduma kwa Wananchi katika eneo moja.
Katika hatua nyingine, Mutatembwa ameipongeza timu nzima ya Wizara inayosimamia ujenzi wa Jengo hilo Kwa usimamizi mzuri unaoleta matokeo chanya ambapo kwa sasa hatua ya ujenzi wa Jengo hilo ni wa kuridhisha na linatarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Katika ziara hiyo, Naibu Katibu Mkuu aliongozana na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Raslimali Watu, Prisca Lwangili, Viongozi wengine wa Menejimenti ya Wizara pamoja na uongozi wa Kampuni inayojenga jengo hilo ya LI JUN.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato