
Na Joyce Kasiki,Dodoma
MBUNGE wa Bukoba Mjini Johnson Mutasigwa ameiomba Serikali kuwapatia wauzaji wa senene masoko pamoja na vifaa vya kutegea senene.
Akiuliza swali Bungeni jijini Dodoma,Mbunge huyo ametaka kujua kama Serikali ina mpango gani wa kufanya hivyo kwa maslahi mapana kwa wananchi wa Bukoba mjini.
“Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapatia wauza senene masoko na vifaa bora vya kutegea senene? ” amehoji Mbunge huyo
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Viwanda Denis Londo amesema, Serikali inaendelea kutafuta na kufungua masoko ya uhakika kwa bidhaa za senene.
“Hii inajumuisha kuwaunganisha wafanyabiashara wa senene na masoko ya miji mikubwa nchini, kuwashirikisha katika maonesho ya biashara ya kitaifa na kikanda, na kutangaza senene kama bidhaa ya kipekee ya Kanda ya Ziwa yenye uwezo wa kuingia kwenye masoko mapana ya Afrika Mashariki na kwingineko. “Amesema Londo
Aidha amesema , Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO), kwa kushirikiana na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) pamoja na VETA, imeendelea kufanya tafiti mbalimbali zinazolenga kuendeleza na kuboresha biashara ya senene katika mkoa wa Kagera.
“Mpaka sasa, teknolojia rahisi ya mfano (prototype) itakayosaidia katika uvunaji wa senene imebuniwa na kutengenezwa.”amesema
Katika swali lake la nyongeza Londo amesema”kwa sasa wauza serene wapatao zaidi ya 1000 jimbo la bukoba mjini hawana eneo mahusus la kufanyia shughuli zao na pembeni yao wanapofanyia shughuli kuna jengo la Kituo kikuu cha mabasi ambalo linaenda kujengwa kwa sasa.”
Ametaka kujua kama serikali haiwezi kutenga fedha kidogo na kuongeza kwenye jengo hilo ili hao wafanyabiashara wa senene wakapata sehemu sahihi ya kufanyia shughuli zao ,.
” Ni lini mheshimiwa waziri ataambatana na mimi kwenda kuona hayo maeneo pia kupata fursa ya kuongea na wafanyabiashara wa jimbo la Bukoba mjini.
Akijibu kuhusi mazingira wezeshi Londo ameaema Serikali ikishirikiana na Manispaa ya bukoba tumeweza kuendeleza mradi wa ujenzi wa soko la serene katika soko la mjini ‘senene complex’
Amesema lengo ni kuwaweka wafanyabiashara wote wa senene pale na kutengeneza mazingira rafiki ambayo yatasaidia katika suala la biashara ya senene .

More Stories
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama