April 1, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mulika Community kusaidia Serikali kukomesha vitendo vya ukatili

Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Dar

SHIRIKA lisilo la kiserikali la kusaidia jamii na waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia limezinduliwa rasmi na Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jery Silaa huku likisisitiza kuisaidia Serikali kukomesha vitendo vya ukatili.

Mwenyekiti wa shirika la Mulika Community Saida Mavumbi,amesema lengo ya shirika hilo kuwaunganisha waathirika wa kijinsia na kuwapa mafunzo ya afya ya akili, kutoa misaada wa kisheria kwa ajili ya kulinda haki na utu wa jamii husika .

Amesema shirika linaisaidia Serikali kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa jamii, kuhamasisha na kutoa tahadhari juu ya mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na kuweka sawa mazingira ikiwemo kupanda miti katika taasisi za umma ikiwemo shule.

Pia litatoa elimu mtambuka kwa jamii iliyoathirika ili kutambua haki zao hususani za watoto wadogo , wafanyakazi wa nyumbani ikiwemo kupata elimu na kupewa uhuru wa kwenda kuchagua viongozi.Pia kutoa mafunzo ya ushonaji nguo, utengezaji wa batiki ,ususi na urembo.

“Shirika letu pia linahamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa jamii na kutoa mafunzo ya cherahani kwa watu 600 ikiwemo wasichana,watu wenye Ualbino na wajane kwa muda wa miezi mitatu,”.

Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jery Silaa,alikabidhi shirika hilo kompyuta kwa ajili ya kusaidia katika shughuli zao huku akiwahimiza kufanya kazi katika kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto na jamii kwa ujumla