Na Mwandishi wetu,Timesmajiraonline,Dar
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limempongeza Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa uzalendo wao uliotukuka kulinda na kutunza tunu za Muungano.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam,jana Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubakar Bin Zubeir, amesema ni wajibu kuwapongeza viongozi hao kwa sababu wameweza kutunza Muungano ambao umeleta umoja na amani kwa Watanzania wote.
Mufti amesema Muungano huo ulituzwa kwa thamani kubwa na waasisi wetu, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.
Aidha, amesema BAKWATA imepokea mwaliko rasmi kutoka Serikalini kuishiriki dua na maombi ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kuliombea Taifa kwa kufikisha miaka 60 ya Muungano.
Amesema dua hiyo itafanyika April 22 mwaka huu mkoani Dodoma ambayo itahusisha waumini wa dini zote na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua