Na Moses Ng’wat, Timesmajira Online,MbozI.
JESHI la Polisi Mkoa wa Songwe linamshikilia mtumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe na Mfanyabiashara ambaye ni mmliki wa maabara ya binadamu kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 40.
Watuhumiwa hao wanaoshikiliwa ni Eliud Mwinyumwe (25) ambaye ni Mtumishi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe kwenye kitengo cha mapokezi wagonjwa wa nje (OPD) ambapo anatuhumiwa kuvunja chumba cha mionzi katika hospitali hiyo na kuiba vifaa tiba kisha kwenda kuvihifadhi kwa Fredrick Mwamlima (25) ambaye ni Mfanyabiashara na mmiliki wa maabara binafsi ya binadamu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya, amewaambia waandishi wa habari kuwa, watuhumiwa hao walikamatwa Oktoba 11, 2023, wakiwa na vitu hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 40 vikiwa ni mali ya serikali kutoka hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe iliyopo Kata kata ya Hasamba wilayani Mbozi.
Kamanda Mallya amesema watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kutokea tukio la uvunjaji katika hospitali ya hiyo ya rufaa lililotokea Oktoba 7, 2023 kisha kuibwa vitu mbalimbali vilivyokutwa kwa watuhumiwa hao.
Mallya amesema mtuhumiwa namba moja (Mwinyumwe) ambaye ni mtumishi katika hospitali hiyo baada ya kukamtwa alikiri kutenda kosa la uvunjaji na kuiba baadhi ya vifaa tiba ambavyo alienda kuvihifadhi kwa mtuhumiwa wa pili.
Amesema baada ya mtuhumiwa huyo wa pili (Mwamlima) ambaye ni mmiliki wa maabara kutajwa, jeshi la polisi lilifanya upekuzi nyumbani kwake mtaa wa Ipanga, Kata ya Ichenjezya,wilayani Mbozi, ambapo alikutwa na dawa mbalimbali za binadamu, pamaoja na vifaa tiba.
Alitaja vifaa tiba vilivyokutwa kwa mtuhumiwa huyo kuwa ni mashine ya ultra sound pamoja na grucomiter, huku vifaa tiba vingine kama printer,centfuge, microscope vilikutwa kwenye maabara anayoimiliki inayojulikana kwa jina la Kamatingo iliyopo mtaa mwingine wa Isangu wilayani humo vyote vikiwa na thamani ya milioni 40.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi