Na Mwandishi Wetu, TimesMajira
MTOTO mdogo wa mwaka mmoja na nusu aliyefahamika kwa jina la Tifan Osward ameuawa kwa kunyongwa shingo na msaidizi wa kazi za ndani (jina limehifadhiwa) ambaye aliachwa nyumbani na mtoto huyo.
Taarifa ya Polisi mkoani Arusha iliyotolewa kwa waandishi wa habari imeeleza kuwa, tukio hilo lilitokea Juni 19, mwaka huu saa 12:00 jioni maeneo ya Olasiti katika jiji la Arusha.
Kwa mujibu wa Polisi taarifa za awali zinaonesha kuwa, binti huyo aliajiriwa miezi miwili iliyopita akitokea Mkoa wa Mara.
“Jeshi Ia Polisi linaendelea kufanya upelelezi ill kubaini chanzo cha tukio hilo,” ilieleza taarifa hiyo na kuongeza;
“Mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi Ia Polisi kwa mahojiano zaidi kufahamu chanzo cha maamuzi hayo na pindi Upelelezi utakapo kamilika jalada litapelekwa Ofisi ya Taifa ya mashtaka kwa uamuzi wa kisheria,”ilifafanua taarifa hiyo.
Kufuatia tukio hilo, Polisi imewataka wazazi na walezi kufuatilia mienendo ya wasaidizi wao wa kazi za ndani kabla na baada ya kuwachukua ili iwasaidie kufahamu tabia zao kwa kina na pindi wanapowachukua wasaidizi hao yasitokee madhara yeyote kwa watoto na familia zao pindi wanapowaachwa majumbani.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua