Na Joyce Kasiki Timesmajira online Dodoma
MTOTO Dominika Mwaluko (miezi 6) ambaye amefariki kutokana na kile kinachosadikiwa ni kulawitiwa na baba yake mzazi amezikwa leo Mbuyuni kata ya Kizota jijini Dodoma huku wananchi walioshiriki katika mazishi wakilaani vikali kitendo hicho.
Akizungumza wakati wa ibada ya mazishi ya mtoto huyo Mchungaji Ova Masebo amesema ni lazima wanadamu warudi pamoja kumtafuta Mungu ili waache vitendo vya ukatili.
“Ujue Mungu alitupenda ndio maana akatuweka duniani kwa hiyo vile unavyoishi ,na mwingine anatakiwa kuishi,vile unaishi na yule uliyemtoa ngozi alitakiwa kuishi ,hakuna mwenye haki ya kuishi kuliko mwenzake,lazima turudi kwa pamoja kumtafuta Mungu kwa hali na mali.”amesema Mchungaji huyo.
Kamanda wa polisi SACPÂ George Katabazi amewahakikishia wananchi kwamba vitendo vya ukatili vinaenda kumalizika mkoani humo.
Naye Mkuu wa mkoa wa Dodoma ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo Rosemary Senyamule amesema tayari mtuhumiwa yupo kwenye vyombo vya sheria na haki ya mtoto Dominica itapatikana.
Steven Mwanga mkazi wa Mbuyuni amesema tukio hilo ni la kuhuzunisha ambalo linahusisha kabisa imani za ushirikina.
Mbunge wa viti Maalum Subira Mgalu amesema kitendo hicho ni cha kulaaniwa na kukemewa vikali.
Mama mzazi wa mtoro hugo Stellah Mlewa amesema tukio hilo lilitokea baada ya baba wa mtoto kuondoka na mtoto majira ya saa mbili usiku September 2 mwaka huu na kisha kwenda kuntelekeza mlangoni nyumbani kwa mkwe (mama wa mke wake).
Amesema baada ya kuona mumewe anachelewa kurudi nyumbani na mtoto alianza kumtafuta na akakutana na balozi ambaye aliampa taarifa za mwanae kwamba ametelekezwa kwa bibi yake ndipo akaenda kwa mama yake na kumkuta mtoto na kutokana na hali aliyokuwa nayo wakaenda polisi na kisha hospitali.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba