January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mtibwa yatengewa bil.1.2/- kupelekewa umeme wa uhakika


Na Mwandishi Wetu

SERIKALI kupitia Wizara ya Nishati imetenga sh. bilion 1.2  ili kujenga njia kubwa ya umeme kuanzia Msamvu Manispaa ya Morogoro hadi kiwanda cha sukari cha Mtibwa kilichopo Wilayani Mvomero mkoani hapa.

Hatua hiyo inalenga kukabiliana na changamoto ya umeme kiwandani hapo.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nishati, Dkt. Merdad Kalemani wakati wa ziara yake ya siku moja kwa ajili ya kukagua changamoto zinazokikabili kiwanda hicho, ambapo alikutana na changamoto ya  kukatika kwa umeme mara kwa mara hali inayosababisha utendaji wa kazi kusuasua.

Baada ya kupata malalamiko mbalimbali ikiwemo changamoto ya umeme,
Waziri Dkt. Kalemani amewatoa hofu wawekezaji wa kiwanda hicho kuwa Serikali imeshatenga sh. bilioni 1.2 ili kutatua changamoto hiyo.

“Kilichonileta hapa ni kuwajengea laini ya kwenu ya kiwanda chenu peke yenu na tumeshapata wataalamu na tumeshaweka bajeti, kwa hiyo Serikali kupitia shirika imetenga sh. bilioni 1.2 kufikisha umeme mkubwa hapa kiwandani,” amesema Dkt. Kalemani.

Kwa habari zaidi soma Majira kesho