Na David John, TimesMajira Online
WATU tisa wakiwemo viongozi wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani humo kwa tuhuma mbalimbali za rushwa.
Taarifa ya TAKUKURU Mkoa wa Arusha iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa TAKUKURU mkoani humo, James Ruge imesema kuwa, watu hao wamekamata kwa nyakati tofauti ambapo wapo pia watumishi wa Serikali na wafanyabiashara.
Imewataja watu hao wanaotuhumiwa kwa rushwa ni Sifael Palangyo ambaye ni Mjumbe wa Baraza la Jumuiya ya Wazazi (CCM), Upendo Ndorosi ambaye ni Katibu wa Malezi Wilaya ya Longido na Mjumbe wa Baraza la Wazazi Mkoa wa Arusha na Laraposho Laizer ambaye ni Katibu wa Wazazi Wilaya ya Longido.
Wengine ni Godwait Mungure ambaye ni Katibu wa Wazazi Kata ya Kikatiti Meru, Mboiyo Mollel ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Tukusi Kata ya Loksare wilayani Monduli,Mikidadi Mollel ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Pembejeo Kijiji cha Tukusi, Kanankira Mnyari ambaye ni Wakala wa pembejeo za kilimo kijiji cha Loit kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Gervas Mollel mfanyabiashara wa Kata ya Oltrumet wilayani Arumeru pamoja na Joseph Christopher Mollel mfanyabiashara katika Kata ya Oltrumet.
Kuhusu makosa wanayotuhumiwa nayo, taarifa hiyo ya TAKUKURU imefafanua kuwa Juni 26, mwaka huu ilipokea taarifa kutoka kwa raia mwema kuwa, Lilian Ntoro ambaye anatarajia kugombea ubunge wa Viti Maalum Wazazi Mkoa wa Arusha alikuwa amempatia fedha Sifael Pallangyo kwa ajili ya kwenda kuwahonga wajumbe wa Baraza la Jumuiya ya Wazazi Walaya ya Longido ili kushawishi kumpigia kura katika kura za maoni.
More Stories
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi