Na Mwandishi Wetu,Timesmajira
MEYA Baraza la Manispa Mjini Unguja,Ali Haji Haji alikutana na kufanya mazungumzo na wakazi wa nyumba mpya za kwahani kwa lengo la kuhamasisha uwekaji wa bustani na maua kwenye nyumba hizo ikiwa ni mapango wa baraza wa kupendezesha Mji.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya kusaidia kupendezesha nyumba hizo,amesema mbali ya kutoa hamasa hiyo pia ametoa miti ya maua 20 kama kuanzia katika kampeni hiyo,bila ya malipo kwa wananchi hao ili kuleta haiba na mandhari mzuri kwenye eneo hilo.
Mstahiki Meya amesema kuwa baraza la Manispa lipo katika kutekeleza mpango mkakati wa upendezeshaji wa Mji hivyo amewataka wakazi wote wa Manispa ya Mjini kuunga mkono mpango huo ili kutoa taswira nzuri kwa wenyeji na wageni.
Aidha Mstahiki Meya aliwataka wakazi wa Nyumba hizo kutunza mazingira na miundombinu iliyopo kwa faida ya kizazi cha sasa na baadae.”Nasikitishwa na hatua ya baadhi ya wananchi ya kuharibu na kuchafua mazingira na haiba ya nyumba hizo,Nyumba ni mzuri na ni za kisasa zinahitaji kutunzwa njia moja ya kuzitunza ni kuwepo kwa bustani,”amesisitiza.
More Stories
5 “best” Bitcoin Online slots games
Best Web based casinos Norway Your own #1 Norwegian Online casinos 2024
Prof. Mwakalila asisitiza uadilifu, uzalendo kwa wanafunzi wapya chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere