Judith Ferdinand,Timesmajira,Online,Mwanza
Zikiwa zimesalia,siku 62,kufanyika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa nchini,unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024,Msimamzi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,Ummy Wayayu,ametoa maelekezo kuhusu uchaguzi huo.
Akizungumza Septemba 26,2024, wakati wa kutoa maelekezo hayo,kwa viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa, na dini,kutoka wilayani Ilemela,mkoani Mwanza,Wayayu ameeleza kuwa, ametoa maelekezo hayo siku 62,kabla ya siku ya uchaguzi,lengo ni kuhakikisha kuwa taratibu zote zinafuatwa.Wapiga kura na wagombea wanapata taarifa zinazohitajika kwa wakati.
Wayayu,ametaja miongoni mwa maelekezo hayo ni pamoja na tarehe ya uchaguzi,ambapo ameeleza kuwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa viongozi wa Mamlaka za za Serikali za Mitaa,uchaguzi utafanyika Novemba,27,2024.
Maelekezo mengine,ni muda wa kuandikisha wapiga kura,ambapo amesema,zoezi hilo litafanyika kwa siku kumi kuanzia Oktoba 11 hadi 20,2024,katika vituo vilivyopangwa,huku akito wito kwa jamii,kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo.
Pia,muda na mahali pa kufanyia uchaguzi,kuwa utafanyika katika vituo vilivyopangwa katika mitaa.Huku maelekezo mengine ni wito kwa wakazi wenye sifa za kupiga kura.Hivyo wakazi wenye umri wa miaka 18 au zaidi,waliokidhi masharti ya kisheria wanahimizwa kushiriki katika uchaguzi huo.
“Wito kwa wagombea,wakazi wenye umri wa miaka 21 au zaidi,wanaotaka kugombea nafasi za Uenyekiti wa mtaa au ujumbe wa Kamati ya Mtaa,wanahimizwa kuchukua fomu za kugombea katika ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi,”amesema Wayayu.
Sanjari na hayo amesema zoezi la kuchukua na kurejesha fomu.Fomu za kugombe,zitatolewa na kutakiwa kurudishwa kuanzia Novemba 1 hadi Novemba 7,mwaka huu kwa Msimamizi wa Uchaguzi.
Aidha amesema,uteuzi wa wagombea utafanyika Novemba 8,2024,huku muda wa kuweka pingamizi kuhusu uteuzi wa wagombea ni kuanzia Novemba 8 hadi 9,2024 na uamuzi wa pingamizi utatolewa kuanzia Novemba 8 hadi 10,2024.
“Rufaa dhidi ya uamuzi kuhusu pingamizi la uteuzi,zitapokelewa,kuanzia Novemba 10 hadi 13,2024,na uamuzi wa kamati ya rufaa utatolewa kuanzia,Novemba 10 hadi 13,mwaka huu,”amesema.
Vilevile,amesema kampeni za uchaguzi zitaanza Novemba 20 hadi 26,mwaka huu kuanzia saa 2 asubuhi hadi 12 jioni,hivyo ametoa wito kwa wananchi wenye sifa kushiriki kikamilifu
Kwa upande wake,Kaimu Katibu wa Chama Cha Kijamii(CCK),Wilaya ya Ilemela,Holela Mabula,.amesema ushirikishwaji imekuwa ukifanywa awamu kwa awamu.
Wanachi wajitokeze,na sisi viongozi wao wa vyama likitokea changamoto tutawajulisha.Tumejipanga kusoma na kuzielewa kanuni za uchaguzi,tulizozipokea leo,na tutakwenda kuzifanyia kazi,na pale itakapotokea mambo yanaenda tofauti na kanuni,tutapaz sauti zeru kuwajulisha wananchi,”amesema.
Mwenyekiti wa DP, Wilaya ya Ilemela,Mch.Clement Pancras,ametoa wito kwa jamii, kushiriki kujiandikisha na kupiga kura,ili kupata fursa ya kuchagua viongozi wazuri,wenye sifa ambao watasaidia ustawi wa nchi na maendeleo ya jamii.
“Wananchi tujitokeze,kujiandikisha kwa wingi,na siku ya kupiga kura tujitokeze,kuchagua viongozi wanaostahili kutuongoza,wenye maono ya kupeleka taifa mbele,”amesema Sheikh wa Wilaya ya Ilemela Abdulwarith Juma.
Huku Katibu Mwenza Kamati ya Amani,Wilaya ya Ilemela, Mchungaji Canon Mlugu,amewataka wananchi kuacha ushabiki,undugu,bali waangalie sifa za mtu kuwa kiongozi atakaye leta maendeleo katika maeneo yao.
“Wananchi wajitokeze kujiandikisha na kupiga kura.Tumeelewa kanuni,tutaenda kuelimisha jamii kuwa uchaguzi siyo vita wala ngumi,bali ni jambo jema na la amani,wachague viongozi sahihi na kutunza amani kwani ikipotea kuirudisha ni ngumu,”.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria