Na Penina Malundo,Timesmajira
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji wa Serikali,Gerson Msigwa amesema Mradi wa Kimkakati wa kufua Umeme kwa maji wa Julius Nyerere(JNHPP) imeanza kuzalisha umeme na kufanya hali ya huduma za umeme nchini kuimarika.
Amesema hadi sasa mradi huo mpaka Februari 2025, mradi umefikia asilimia 99.8 na kubakiza asilimia 0.2 kukamilika kwake.
Akizungumza leo Mkoani Pwani wakati akiongea na waandishi wa habari,Msigwa amesema kutokana na hali hiyo hali ya upatikanaji wa nishati ya umeme nchini kwa sasa imefikia asilimia 78.4.
Amesema mradi wa JNHPP umeongeza uwezo wa kuzalisha umeme katika Gridi ya Taifa ambapo wakati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani Machi 2021, mradi ulikuwa asilimia 33 mpaka Februari 2025, mradi umefikia asilimia 99.8.

“Mpaka sasa, jumla ya mashine 8 kati ya 9 zimeshawashwa na kufanya jumla ya MW 1,880 kuongezeka kwenye Gridi ya Taifa ya Umeme.”Utekelezaji wa mradi wa kusafirisha umeme kutoka JNHPP hadi Chalinze kV 400 wenye urefu wa KM 160, umefikia asilimia 99.5 ikilinganishwa na asilimia 44 mwaka 2021/22,”amesema
Amesema ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Chalinze ambacho ni sehemu ya mradi wa JNHPP umefikia asilimia 92 ikilinganishwa na asilimia 35.9 mwaka 2021/22.
“JNHPP imeanza kuzalisha umeme na kufanya hali ya huduma za umeme nchini kuimarika. Uwezo wa uzalishaji wa umeme kutokana na mitambo iliyounganishwa kwenye gridi ya taifa ni MW 3,796.71.

” Matumizi ya juu yaliyofikiwa ni MW 1,900.62 iliyofikiwa tarehe 14.2.2025, ikiwa ni ongezeko la MW 124.22 kutoka MW 1,776.4 za Novemba mwaka 2024,”amesemaAmesema matarajio ya uzalishaji umeme kufikia mwisho wa mwaka 2025 yatakuwa MW 4,081.71,ongezeko litatokana na kukamilika kwa JNHPP mashine ya mwisho na MW 50 za umeme wa jua kwenye mradi wa Kishapu).
“Matarajio ni kuzalisha MW 7,992.5 ifikapo mwaka 2030,”amesema
More Stories
Wanawake Kisukuru kuwezesha kuku kujiinua kiuchumi
21 washikiliwa kwa tuhuma mbalimbali akiwemo mwenyekiti wa mtaa, kitongoji
Wananchi wamuunga mkono Prof.Muhongo uvuvi wa vizimba