December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

MSIBA WA TAIFA BURIANI RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza siku 7 za maombolezo ya Kitaifa kuanzia leo Ijumaa tarehe 24 Julai, 2020 kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa kilichotokea Jijini Dar es Salaam.

Katika kipindi chote cha maombolezo bendera zote zitapepea nusu mlingoti.

Rais Magufuli amewaomba Watanzania wote kuendelea kuwa watulivu, wastahimilivu na wamoja katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao, Rais Mstaafu Mkapa.