December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mhariri wa Gazeti la Mawio, Jabir Idrissa

Mshtakiwa kesi ya Lissu awekwa karantini Z’bar

Na Grace Gurisha

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa aliyekuwa Mhariri wa Gazeti la Mawio, Jabir Idrissa anayekabiliwa na kesi ya kuandika habari za uchochezi, yupo kwenye uangalizi Visiwani Zanzibar.

Mbali na Jabir washtakiwa wengine ni aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, aliyekuwa Mhariri wa gazeti la Mawio, Saimon Mkina na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.

Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa, lakini mshtakiwa Jabir yupo karantini na Lissu hayupo mahakamani na hakuna taarifa zozote mpya kumuhusu.

Wadhamini wa Lissu, Robert Katula na mwenzake walikuwepo mahakamani hapo. Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 2, mwaka huu.