Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online, Kagera
MKAZI wa Bukoba mkoani Kagera, Maclina Romward Rugeiyamu, mwishoni mwa wiki alikabidhiwa zawadi ya jembe la kutumia teknolojia ya kisasa (Power Tiller) alilojishindia kupitia promosheni inayoendelea ya bia ya Balimi Extra Lager.
Promosheni hiyo ya wiki nane iliyozinduliwa mwezi uliopita inawezesha wateja wa bia ya Balimi kujishindia Power Tiller, muda wa maongezi, bia za bure, na T-shirts.
Meneja wa bia ya Balimi,Pamela Kikuli akiongea wakati wa hafla hiyo,aliwataka wakazi wa kanda ya ziwa ambako promosheni hiyo inafanyika kuendelea kunywa ya Balimi na kutuma tarakimu watakazozikuta chini ya kizibo kwenda namba 15054 ambapo zitaingizwa kwenye droo ya wiki inayofanyika kupitia luninga ya Star .“ Bado kuna power tiller sita hazijapata washindi na zawadi nyingi za vocha za muda wa maongezi,hivyo wateja wenu wanayo fursa ya kuchangamkia zawadi hizi”alisema.
Naye Maclina Rugeiyamu alitoa shukrani kwa kampuni ya TBL kwa kubuni promosheni zenye malengo ya kunufaisha weateja wake “Zawadi hii itaniwezesha kuendesha kilimo cha kisasa kitakachowezesha kujiongezea kipato na kuboresha maisha yangu na familia.
More Stories
Wanafunzi 170 wapata ufadhili wa masomo
Maelfu kunufaika namsaada wa kisheria Katavi
Serikali yazidi kuwakosha wawekezaji wadau waipa tano