Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online.
MSANII maarufu wa Bollywood, Sanjay Dutt amethibitisha kuwa ana saratani baada ya minong’ono ya wiki nzima iliyovuma katika vyombo vya habari nchini India.
Katika video ya mtandao wa Instagram, msanii huyo mwenye miaka 61, ambaye ameshashiriki katika filamu zaidi ya 150, amesema “nitaushinda ugonjwa huu hivi karibuni”. Dutt anasema ataanza kuandaa sinema nyingine mwezi ujao (novemba).
Kwa mujibu wa taarifa ya BBC, mwezi Agosti, 2020, Dutt alizushiwa kuwa na virusi vya Corona ambavyo vinasababisha ugonjwa wa Covid-19, baada ya kuripotiwa kuwa na changamoto ya upumuaji. Lakini vipimo vilionesha hakuwa na ugonjwa huo.
Pamoja na Corona pia alipimwa magonjwa mengine katika hospitali jijini Mumbai. Lakini kufuatia taarifa ambazo hazikuwa zimedhibitishwa, alikutwa na saratani ya mapafu, ambapo Sanjay alisema “nachukua mapumziko mafupi ya kazi kwaajili ya matibabu”
Mke wa muigizaji huyo, Maanayata, alitoa taarifa kwa wanahabari, akiwaondoa wasiwasi mashabiki wa nyota huyo “puuzeni uzushi huo” kuhusiana na hali yake.
Video ya mwihso iliyorekodiwa Dutt akiwa kwa kinyozi wake, Aalim Hakim, ambapo alionesha jeraha kubwa linalotokea kwenye kiwiko cha mkono wake wa kushoto mpaka kichwani.
“hili ndio kovu la maisha yangu. Lakini nitashinda tu. Nitaishinda saratani muda si mrefu” alisema Sanjay na kuongeza kuwa anafuraha kushiriki tena kwenye filamu ijayo
Dutt (pichani kushoto akiwa chini ya ulinzi) alifahamika Bollywood kwa umaarufu wake wa kushiriki katika filamu mbalimbali ambapo ghafla alipotea baada ya kutakiwa kumalizia hukumu ya kifungo cha miaka mitano mwaka 2013 baada ya kukutwa na hatia ya kukutwa na silaha iliyohusishwa na mlipuko wa mwaka 1993 jijini Mumbai ambao uliua watu 257 na kujeruhi wengine 713.
Hata baada ya kifungo hicho alifanikiwa kuibuka tena mwaka 2016 alipotoka jela. Dutt alisaini mikataba ya filamu kadhaa ambazo baadhi zilifanya vizuri sana katika box office.
Msanii huyo pia aliongelea wazi matatizo yake ya urtaibu wa dawa za kulevya baada ya kushambuliwa katika mahojiano na waandishi wa habari na kusema kuwa matatizo hayo yamempa ujasiri mkubwa
Dutt pia amepoteza ndugu wawili katika familia yake kutokana na maradhi ya saratani, ambapo mama yake, Nargis mwaka 1981 alipoteza maisha kwa saratani ya kongosho siku chache kabla ya Dutt kufanikiwa kuingia katika fani ya uigizaji filamu Bollywood. Mwingine ni mkewe wa kwanza Richa Sharma aliyekufa kwa saratani ya ubongo.
More Stories
Rais Samia atia mkono mchezo wa masumbwi Tanzania
Dk. Mpango amwakilisha Samia sherehe za Uhuru wa Lesotho
Chino bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship