Na Bakari Lulela,Timesmajira
MSANII wa muziki wa singeli nchini Divorce anatarajia kufanya onesho kubwa katika ukanda wa ziwa kuanzia juni 6 atakuwa maeneo ya shinyanga, juni 7 Nyamongo katika ukumbi wa Friday club na juni 8 atakuwa maeneo ya mwanza.
Akizungumza jijini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari Divorce amesema anajivunia kutembelea lebo ya Wasafi hivyo na kuwataka mashabiki wake kukaa tayari na shoo kabambe.
“Nawashauri wapenzi wa muziki wa singeli kukaa mkao wa kula Ili kupata burudani wa muziki huo pia mandasi store watakuwa wakitoa huduma ya simu kwa mkopo maalumu,” amesema Divorce
Aidha nawaasa wapenzi wotewa burudani kujitokeza maeneo hayo kwa lengo la kujipatia huduma ya simu kwa mkopo Ili waweze kupata kifaa muhimu kitakacho rahisisha mawasiliano.
Nae mdhamini wa msanii huyo Hamisi Manda’s amesema kuwa amesema kutumia mwanamuziki huyo kwa kuwa muziki wake umekuwa ukipendwa sana na jamii kwa mashairi yake mazuri.
Hata hivyo tumeamua kumchagua msanii huyu kwa kuwa anaonekana kuwa na mvuto kwa wapenzi wa muziki hapa nchini na Duniani kwa ujumla .Ili iweze kupata mikopo huo inatakiwa kuwa na kitambulisho cha kura, Taifa ama ,leseni itakuwezesha kupata mikopo huo
Kwa upande wake msanii ambaye ni msimamizi wake Baba levo amesema kuwa msanii Divorce anajivunia weledi wa mashairi yake ambapo amekuwa akipendwa na mashabiki wake anaimba muziki wa singeli. Hivyo ukija kwenye muziki wa Divorce njoo na kitambulisho chako cha Taifa, leseni Yako, kitambulisho cha kura
More Stories
Kiongozi wa Mwenge apongeza wananchi kupelekewa huduma ya maji Handeni
TFS yawakaribisha wawekezaji katika vivutio vya utalii wa misitu
Waziri Bashungwa:Tumieni teknolojia za kisasa kudhibiti uhalifu unaovuka mipaka