January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Msama: Rais Dkt. Samia anafanya kazi nzuri na kuinua uchumi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kufanya kazi nzuri na kubwa kwaajili ya kuinua uchumi wa nchi hasa katika kuleta wawekezaji wengi nchini.

Aidha Rais Dkt. Samia amehakikisha Wafanyabiashara wa Kariakoo wanafanya biashara zao kwa amani na utulivu.

Hayo ameyasema na Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama wakati akizingumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, na kusema kuwa juhudi za Rais Samia zimepelekea Mamlaka ya mapato Tanzania TRA kukusanya Kodi vizuri bila kuvunja sheria yoyote na kupelekea kuongeza pato la Taifa.

“Rais Dkt. Samia amefanya mambo makubwa sana, ameinua uchumi wa nchi, sasahivi TRA wanaongea vizuri na wafanyabiashara na wanampa mfanyabiashara haki yake, wanakusanya Kodi yao viziri, hawamuonei mtu yoyote”

“Rais Dkt. Samia anatembea kwenye nchi mbalimbali kuhakikisha wawekezaji wote wanakuja kuwekeza nchini, wapo watu ambao hawana nia njema na nchi yetu ya Tanzania, wapo watu ambao hawapendi kuona nchi yetu inaendelea bali kuona matumbo yao yanaendelea hivyo Rais anapohangaika kutafuta wawekezaji ajue kwamba anapambana na watu ambao wanafanya uwekezaji kwenye matumbo yao, namuomba Rais afanye kazi na asiogope ikiwezekana awashughulikie watu hao wanaorudisha nyuma maendeleo ya nchi”

Aidha Msama amewaomba wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya.

Pia amewaomba viongozi wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupeperusha sera nzuri za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

“Msikae kimya na Wala msiwe nyuma katika mapambano ya kuhakikisha kwamba uchumi wa nchi yetu unakua, fanyeni kazi yenu kwa manufaa ya nchi yetu”