December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Msama alazwa JKCI

Na Mwandishi wetu, Timesamajira Online

Mkurugenzi wa Msama Promotions na muandaaji wa Matamasha ya Injili nchini ambaye ni mdau mkubwa wa maendeleo ya sanaa Alex Msama amelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akisumbuliwa na maradhi.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Mkurugenzi huyo amesema siku chache baada ya kumalizika kwa tamasha la Injili la Pasaka lililofanyika katika Viwanja Vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam,na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali nchini wa Kiserikali na wa kidini aliugua ghafla na kulazwa katika hospitali yai taasisi ya Moyo ya JKCI ambapo amesema kwa sasa anaendelea na matibabu.

Akizungumzia kwa sharti la kutotajwa jina alisema Msama anaendelea vizuri ambapo amewaomba waumini na viongozi wa dini achungaji na maaskofu,na Masheikhe wamuombee ili aweze kupona mapema ili kuendelea na kushughuli zake ikiwemo muendelezo wa Matamasha yake ambayo alitarajia kuyafanya katika mikoa mbalimbali nchini

Hivi Karibuni Mkurugenzi huyo aliandaa Tamasha kubwa la Pasaka ambalo lilifanyika katika Viwanja vya leaders Club ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari, ,Mawasialino ya Habari na Tekonolojia ya Habari Nape Nnauye ambaye pia alitumia tamasha hilo kutoa ujumbe mzito wa Serikali juu ya kupinga mapenzi ya jinsia moja ambapo alisisitiza kwamba Serikali inalikemea jambo hilo.

Kwa taarifa zaidi tunaendelea kufuatilia kujua tatizo linalomsumbua Mkurugenzi huyo…