Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dodoma
MWEYEKITI wa Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) mkoani Dodoma, Tryphone Mkolokoti ambaye pia ni MNEC wa TRCS ameongoza zoezi la kugawa msaada kwa waathirika wa ukame wilayani Longido,mkoani Arusha.
Utoaji wa msaada hui ni awamu ya pili kwa waathirika hao kwani mingine imetolewa mkoani Manyara katika Wilaya ya Simanjiro na Mbulu.
Akimwakilisha Rais wa TRCS, Mh. David Mwakiposa Kihenzile (MB), MNEC Mkolokoti ametoa pole kwa wananchi hao jamii ya kifugaji kwa kupoteza mifugo yao kwa ukame na amewaahidi kuendelea kuwa nao pamoja wakati wote wa maafa.
Amewaomba waendeee kuishi katika imani ya TRCS na wawe wanachama wa mfano ili kuweza kuwa karibu katika shughuli za kusaidiana pale wanapoihitaji.
Vilevile TRCS imetoa msaada wa vyakula dawa venye virutubisho muhimu kwa watoto chini ya miaka mitano kutoka jamii hiyo ambazo familia zao zimeathirika na ukame na watoto wao kupata utapiamulo ambapo jumla ya kaya 150 zimepata vyakula hivyo.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu