Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na Frederic Van de vyver Mkuu wa Jeune Afrique Media Group, kampuni inayoongoza ya habari ya ki-panafrika yenye makao yake makuu jijini Paris, Ufaransa.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, wamejadiliana ni kwa namna gani wanaweza wakafanya kazi pamoja katika fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini.

Mchechu amemhakikishia De vyver kuwa Tanzania ina mazingira mazuri ya uwekezaji na kwamba atapata ushirikiano wa kutosha.
“Kwa upande wa sekta ya umma utapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Ofisi ya Msajili wa Hazin ana kwa upande wa sekta binafsi utapata ushirikiano kutoka kwa CEOrt,” amesema Mchechu.

Kwa upande wake De vyver ameeleza dhamira yake ya kuimarisha ushirikiano na Tanzania.“Lazima tutafute namna bora ya kushirikiana,” amesema.


More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina