January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mradi wa “OCP SCHOOL LAB” wazinduliwa Songea

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kampuni ya OCP Afrika iliyo kinara katika uzalishaji wa mbolea ulimwenguni, imezindua rasmi mradi wa “OCP School Lab” kusini mwa Tanzania katika mkoa wa Ruvuma mradi unaolenga kutoa elimu kwa wakulima juu ya afya ya udongo, mbinu sahihi kwa mazao husika.

Uzinduzi wa mradi huu umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya “Heritage Cottage” uliopo mjini Songea Mei 12, 2022 na kuhudhuriwa na viongozi wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na wilaya zake  na walijionea teknolojia juu ya ukemia wa udongo na mapendekezo ya mbolea kutokana na aina ya udongo husika lengo likiwa ni kuogeza tija kwenye kilimo, ubora na ustawi na mazao.  

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa Ndugu Joseph Mkirikiti,  Mkuu wa wilaya ya Kalambo Ndugu Kalolius Misugwi alisema, “sekta ya kilimo imeajiri namba asilimia 65% ya watanzania wote na imelihakikishia taifa upatikanaji wa chakula kwa asilimia 100% pamoja na malighafi za viwandani, lakini bado idadi hiyo ya watanzania wanaojishughulisha kilimo haipo katika uwiano sawa na idadi ya watanzania wote nah ii ni kwa sababu ya tija ndogo inayotokana na uzalishaji mazao. Hiyo mpango huu utasaidia kuongeza na tija na bila shaka kuongeza uzaishaji wa mazao ya kilimo”

“Niwapongeze sana kampuni ya OCP Afrika kwa kuandaa mradi huu ili kusaidia kutathimini rutuba ya udongo katika ngazi yamkulima kwa vijiji 400 katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa na Morogoro na kwamba kazi hiyo itafanyika bila malipo yoyote”. Aliongeza Ndugu Misungwi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo wa mradi wa awamu ya tatu mjini Songea, Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya OCP Tanzania Dkt. Mshindo Msolla alisema, “OCP Tanzania ikishirikiana na Serikali imeandaa mchakato wa upimaji wa udongo kwa zaidi ya vijiji 100 ndani ya mkoa wa Ruvuma.

Lengo ni kuwaelimisha wakulima juu ya udongo wa eneo lao bila gharama zozote kwa wakulima hao. Majibu yatatolewa kwao na kwa kushirikiana na Taasisi ya utafiti wa Kilimo (TARI) tutatoa ushauri wa kitaalamu juu ya nini kifanyike ili kutunza ubora wa udongo wa kijiji husika kwa matokeo bora ya shughuli za kilimo. Katika kila kijiji zaidi ya wakulima 100 watafikiwa na kuelimishwa namna bora za kufanya kwa mradi huu tunazamia kufikia wakulima 10,000 kwa mkoa wa Rukwa pekee.

Mradi huu wa upimaji na tathmini ya udongo kwa mwaka 2022 unatarajiwa kuendeshwa katika vijiji 600 na kuwafikia wakulima wapatao 60,000 kufikia mwisho wa mwaka 2022. Mradi huu pia unatarajiwa kutoa tathmini ya udongo na mapendekezo ya matumizi ya mbolea kwa wakulima wapatao 12,000 watakao wakilisha wakulima wenzao kutoka mashamba mbalimbali kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

“Ni jambo lenye ulazima, kwamba wakulima wetu wawe rafiki wa teknolojia za kisasa zitakazowawezesha kuongeza uzalishaji wao, na hivyo kuondokana na umasikini. Mradi huu wa upimaji na tathmini ya udongo ni jambo la kipekee sana na hivyo tunahamamisha wakulima wote wawe sehemu ya mradi huu”. Aliongeza Dkt. Msolla.

Tangu mwaka 2017 zaidi ya wakulima 430,000 wamenufaika na miradi ya upimaji na tathmini wa udongo kutoka nchi nane barani Afrika za Naijeria, Togo, Ghana, Guinea, Kenya, Burkina Faso, Cote D’Ivoire na Senegal na kwa namna ya kipekee Tanzania inaungana na nchi hizo kuwa moja wa nchi wanufaika wa mradi huo.

Mradi huu wa upimaji na tathmini ya udongo kwa mwaka huu wa 2022 unaratibiwa kwa ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya kilimo, Tawala za mikoa na Serikali za mitaa pamoja na Taasisi ya utafiti wa Kilimo (TARI) wataalamu wa maendeleo ya kilimo.

“Mradi wa upimaji na tathmini wa udongo unaoongozwa na OCP kwa sasa ni nyenzo madhubuti kwa wakulima utakaokua na msaada mkubwa kwa kuongeza kiwango cha uzalishaji mazao”.

Mradi wa OCP SCHOOL LAB Utatoa ushauri sahihi kwa mkulima mmoja mmoja na mapendekezo yanayolenga kuongeza  tija ya  mazao kama mahindi, mpunga, soya, miwa, ngano, maharage, kahawa, pamoja na alizeti.

Mradi huu ni mwendelezo wa awamu mbili zilizotekelezwa mwaka 2019 na 2021,na kufikia wakulima na wadau wa kilimo 60,000 katika mikoa ya Njombe, Rukwa, Iringa, Mbeya, Morogoro na Songwe. Majibu ya utafiti wa udongo kwenye mikoa hii yameweka bayana kwamba ukiachia mbali upungufu wa madini ya Fosforas na Naitrojeni uliopo kwa kipindi kirefu, kuna upungufu pia wa madini ya Zinki, Salfa, Boroni pamoja na Potasiamu.

OCP Afrika kupitia kampuni tanzu ya OCP Tanzania  ilizindua awamu ya kwanza ya mradi wa tathmini ya udogo mwaka 2019,na awamu ya pili mwaka 2021, na awamu hii ya tatu ya mradi huo unatarajiwa kuhudumia wakulima na wadau wa kilimo wa mikoa ya Ruvuma, kufuatiwa na Katavi, Kigoma, Manyara, Arusha and Kilimanjaro kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Idara za Kilimo (taasisi ya utafiti wa kilimo (TARI) kituo cha Uyole), tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI).

Kuhusu OCP Afrika: OCP Afrika ilianzishwa mwaka 2016 ikifanya kazi bega kwa bega na wakulima ili kuleta maendeleo ya Kilimo. Tunazalisha mbolea za aina mbalimbali zinazoendana na uhitaji wa mazao husika, na tunafanya kazi pamoja na washirika mbalimbali zikiwemo serikali za kitaifa, taasisi na mashirika binafsi ili kuwaunganisha wakulima na mahitaji yao, ufahamu na mallighafi ili waweze kufanikiwa