Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
Mradi wa chanzo kipya cha maji Butimba kinatarajiwa kuanza majaribio ya utoaji maji Septemba 15, mwaka huu huku ujenzi wake ukiwa umefikia asilimia 94.
Ambao unathamani ya bilioni 69, utaenda kutatua changamoto ya maji kwa wakazi wa jijini Mwanza kwa kiwango kikubwa hivyo kuondokana na hadha iliyopo sasa.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ambaye ameeleza kuwa kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi huo kutaongeza upatikanaji wa maji kutoka lita milioni 90 kwa siku za sasa hadi kufikia lita milioni 138.
Aweso amesema mradi huo utanufaisha wakazi wa maeneo ya Nyegezi, Mkolani, Buhongwa, Nyamazobe, Nyahingi, Buganda, Luchelele, Lwanhima, Sahwa, Fumagila, Kishiri na Igoma kwa upande wa Jiji la Mwanza.
Kwa upande wa Wilaya ya Misungwi alitaja maeneo ya Usagara, Nyashishi na Fella wakati kwa upande wa Magu ni Kisesa, Bujora na Isangijo.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi